Sunday, July 27, 2008

KAGAME CUP

Aibu ya kihistoria!!!!!!
Klabu ya Yanga imegomea kuingiza timu uwanjani kupambana na Simba katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa Kombe la Kagame uliokuwa upigwe katika uwanja mkuu wa Taifa.

Hii ni mara ya kwanza tangu michuano hii ya Klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati kwa timu kugomea mchezo.

Yanga pamoja na Simba zilikuwa zimeibana CECAFA kuzipa kila moja shilingi milioni 50 kwa vile zenyewe huwa zinaingiza mapato mengi katika michuano hii. Hata hivyo kwa mujibu wa kanuni zinazoongoza michuano hii, mapato huwa hayawahusu vilabu. Kwa hali hii TFF imekuwa ikivisaidia vilabu vinavyowakilisha nchi ili viweze kufanya vizuri.

Mapema leo asubuhi timu hizo mbili zilitokea katika pre-match meeting na katika hali ya ambayo ilionekana kwamba kuna makubaliano ambayo yalikuwa yamefikiwa. Lakini katika hali ya kushangaza Yanga haikutokea uwanjani na Simba ambayo ilionyesha kuheshimu muda wa watu waliojitokeza na hali ya kimichezo iliingiza timu uwanjani.

Simba ilikamilisha taratibu zote na kusubiri kwa dakika 45 (badala ya 15) ndipo ikapewa ushindi dhidi ya Yanga katika mchezo wa leo.

Hapa tunajuliza , hivi kweli Yanga tuna viongozi wa mpira? Hili ni jambo la aibu sana katika maendeleo ya soka kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. CECAFA na TFF inahangaika kutafuta wadhamini halafu tunaishia kukimbiza timu? Inasemekana TBL ilikuwa kupitia bia yake ya Castle ilikuwa iendelee na mkataba mrefu kwa michano hii lakini kwa ujinga huu tutapata wapi wadhamini?

CECAFA itatoa uamuzi kuhusu sakata hili leo jioni.

19 comments:

Anonymous said...

mwenyekiti ni mwanasheria, hapo sasa kazi kweli kweli

Anonymous said...

Wewe ulitegeme nini viongozi wanadai wamekimbia aibu.Mimi ni Yanga kwa mujibu wa kiongozi moja aliyekwenda kuchungulia anadai kwamba tungeingiza timu tungepigwa bao.Hivyo wao viongozi wameona heri lawama kuliko fedhaha.Hao ndio vingozi tuliowachagua na tunategemea maendeleo.

Anonymous said...

ndivyo sivyo ,nina wasiwasi na uwanasheria wa madega iweje msomi awe mpuuzi?akianani aliyesema yanga mgongo wazi hakukosea,ila viongozi wa yanga wajue michezo ni furaha upendo na amani ,mizengwe TUMECHOKA SASA

Anonymous said...

Mechi ya URA na Tusker matokeo vipi??Sisi wengine ni wapenda mpira .

Anonymous said...

Wanachama na wapenzi wa Yanga tunatakiwa tulaani kwa nguvu zote kitendo cha viongozi wetu kuamua kutopeleka timu kucheza na Simba.Licha ya kwamba ni kosa la kiwanamichezo pia ni uoga wa wazi.Kwani hata kama tungefungwa ingekuwa nini??Je tungeingia fainali na Simba wangejitoa????Wanaynga tuamkeni hatuna viongozi tuna wasanii.

Anonymous said...

Kudadadeki, sasa kinachofuata ni bakora tu jangwani. Hatuna viongozi bali wasanii wa soka. Wanaogopa nini! kufunga au kufungwa ni sehemu ya mchezo. Nimesikitika sana.

Anonymous said...

aibu tupu kujiita mwanayanga

Anonymous said...

Hayo ndiyo matatizo ya kuwa na viongozi wanaoendekeza ushirikina. Kamati ya ufundi imeambiwa na babu kuwa leo Yanga hatutoki, basi wao wakaamua kuikimbiza timu! Madai yao ya eti wapewe fedha 50m kabla ya mechi hayana mantiki yeyote. Kwanza zitoke wapi? Na hata zingekuwepo, wapewe kwa sheria ipi ya mashindano? Madega kweli ni mwanasheria au pumba tu! Sasa lazima kieleweke klabuni. Aibu hii tutaipeleka wapi sis Yanga baada ya kutumia mamilioni ya Manji kusajili wachezaji?

Anonymous said...

Waungwana tumesoma maoni yenu, mimi pia siafiki kitendo cha kutoipeleka timu uwanjani,lakini pia siafiki hii lugha ya matusi ambayo naiona humu, nafikiri ni hekima zaidi kujadili mambo kiungwana kuliko hizi lugha zisizo za kiungwana. Badala ya viongozi kuonekana wabovu sasa inaonekana hata wapenzi tuna matatizo. Nilazima tujifunze kuvumiliana na kutatua matatizo kiungwana kuliko hali ninayo iona. Vinginevyo watu wataacha kusoma hii blog kwa kudhani ni ya kihuni.Inahitaji uvumilivu na hekima.

Anonymous said...

namna hii mandeleo jangwani ni ndoto hivi hata kama tungeingia fainali ungefanya hivi...? kwani kabla mashindano hayajaanza viongozi walikuwa haqwajui kuhusiana na mgao .... hii ni aibu ya mwaka hata tukifungiwa miaka 10 na cecafa ni na-support

Anonymous said...

YUSUF MANJI,TAFADHALI SANA TUMIA FEDHA ZAKO MAHALI PENGINE,SIDHANI HAWA VIONGOZI WANA KUELEWA.

Anonymous said...

MGONGO WAZI KAKIMBIA.HAOOOOOOOO BARUTI.MNYAMA NOMA WEWE.

Anonymous said...

But pamoja na yote nafikiri TFF na baraza zima la soka la africa masharika ni wababaishaji, mnakumbuka yanga walivyoteswa kupata hela la kuwa mabingwa? Ukanda huu mpira hauwezi kukua ni ubabaishaji mkubwa kwa kila pande marefa wanachezesha kinazi basi ni taabu tupu. Wadhamini wanatakiwa kuingia mkataba na klabu na wala siyo kuwapa viatu na majezi hizi timu zinaingia gharama mno hivi gharama ya kukaa hotelini ilikuwa inalipwa na nani?

Anonymous said...

Zilikuwa zinalipwa na CECAFA.Tuache kutetea ujinga.Tuliposhiriki kwenye mashindano haya tulikuwa tunajua wazi sheria zake.Wadhamini waingie mkataba upi na klabu.Kuna wanaondesha mashindano sio klabu.Klabu zinajua sheria na kanuni za mashindano hayo kwamba wanalipiwa malzi na nauli.Msindi wa kwanza anapata dola thelathini alfu, wapili ishirini na watatu kumi.Tulipofungwa ndio tukaja na madai mengine.Hivi tungeshinda ingekuwaje tungedai gate collection? Manji aliwaambia viongozi wetu wakifungwa na Simba udhamini basi.Labda ndio sababu ya wao kuingia mchecheto wa kuingiza timu.

Anonymous said...

Kumbe ni Mnaji aliyeamuru timu isicheze sasa viongozi wa nini???

Anonymous said...

Mhh basi afadhali mpeni Jezi huyo Manji acheze first 11 labda mtafanikiwa kuwafunga Simba...acheni ubabaishaji Yeboyebo mpria unachezwa Uwanjani na siyo magazetini...kubali kamwe hamtaifunga simba....

Anonymous said...

miaka mitatu? kufungiwa tumeonewa aisee. lakini mi naona ile fain waliyotupiga utajilipa yenyewe kwenye lilr deni tunalowadai CECAFA

Anonymous said...

aisee, mimi ni mwanachama na mpenzi mkubwa wa YANGA, kwakweli tangu siku ya kutofika uwanjani hata chakula hakipiti, yaani kila ninapopita ni kujitetea tu utadhani mie ndio sijapeleka timu, sasa hii ni nini?

Mimi nadhani wanachama na wapenzi wa soka tubadilike sana, CECAFA, TFF, YANGA, wote wana makosa fulani haiwezekani CECAFA wakubali walikutana na timu 2 hizi, wakiwa na TFF kwa maana gani, hapa ilikuwa na fedha zaidi kuliko burudani na maendeleo ya soka Afrika Mashariki na Kati.

Na hii kusema kuifungia Yanga ni hasira tu, mimi nadhani kama ilivyo FIFA, CAF na CECAFA nao waweke REGULATIONS zao kwatika mtandao ili na sisi tujue hata ni kitu gani cha kushauri kwa timu zetu si kwa YANGA tu hata Manyema nakadhalika, maana CECAFA wanadai yao, YANGA yao, TFF yao ujanja ujanja tu tunapigizwa vichwa, kuna maana gani sasa ya kuwa na mashindano kama wao wenyewe hawaeleweki, mi nachukia wewe
Robert B.

Unknown said...

Sisi yanga ni wajinga sana