Wednesday, August 06, 2008

Simba na Yanga Oktoba 25

Shirikisho la soka nchini TFF limetoa ratiba ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2008/09 ambapo vigogo vya soka nchini Simba na Yanga vitaumana Oktoba 25 kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, ligi hiyo itaanza Agosti 22 kwa Simba kupambana na timu iliyopanda daraja msimu huu ya Villa Squad. Yanga inatarajiwa kukata utepe wa ligi hiyo siku inayofuata kwa kuikaribisha na Tanzania Prisons ya Mbeya.

Ligi hiyo inayoshirikisha timu 12 inatarajiwa kumalizika Aprili 19 2009.

Timu zitakazoshiriki ligi hiyo ni Yanga, Simba, Prisons, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Polisi Dodoma, Polisi Morogoro, JKT Ruvu, Toto Africa, Moro United, Villa Squad na Azam FC.

6 comments:

Anonymous said...

Safari hii mchomoe tena!

Anonymous said...

ahh kumbe unajua.

Anonymous said...

Mkutano umeisha salama?tujulisheni tulio mbali

Anonymous said...

Ulitegemea nini??Bakora zitembee??

Anonymous said...

mdomo mali yako sio wote wahuni

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___