Friday, September 12, 2008

Janja ya nyani...........
Baada ya Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Imani Madega kutangaza kuurudisha nyuma mkutano wa wanachama kutoka Jumapili hadi Jumamosi wiki hii, baadhi ya wanachama wamemshtukia kiongozi wao huyo wakidai amefanya hivyo ili kupitisha kwa nguvu agenda hasa zile zinazolenga maslahi yake binafsi.
Wanachama hao wamesema kuwa kesho watamshinikiza Mwenyekiti wao huyo ili mkutano huo usogezwe mbele kwani siku hiyo timu yao inacheza na Mtibwa Sugar mjini Mororgoro, hivyo hawatapata muda wa kutosha kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya klabu yao kwa sababu watataka kuharakisha kila jambo ili wawahi kwenda Morogoro.
Mkutano wa Yanga awali ulipangwa kufanyika Jumapili lakini ghafla juzi Madega alitangaza kuwa utafanyika kesho jambo ambalo linazua maswali mengi kutoka kwa wanachama na mashabiki wa timu hiyo.
Tangu waingie madarakani mwezi Mei mwaka jana, uongozi wa Madega haujawahi kufanya mkutano mkuu wa wanachama mbali ya ule uliofanyika mwezi uliopita ambao ulikuwa na agenda moja tu ya kupitisha rasimu ya katiba ya klabu hiyo. Mkutano huo ulichukua dakika 40 tu.

1 comment:

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___