Tuesday, October 28, 2008

Ivo bado yupo yupo kwanza Ethiopia


Uhamisho wa kipa wa zamani wa Yanga, Ivo Mapunda kwenda kukipiga katika klabu ya St. George ya Ethiopia bado upo mashakani kufuatia Shirikisho la soka nchini TFF kutotuma hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC) nchini Ethiopia hadi hivi sasa.


Kutotumwa kwa hati hiyo kunasababishwa na TFF kusita kufanya hivyo kutokana na Shirikisho la soka nchini Ethiopia (EFF) kufungiwa na Shirikisho la soka Duniani (FIFA).


Hata hivyo katika juhudi za kutafuta ufafanuzi wa suala hilo, TFF tayari imewasiliana na Shirikisho la soka Afrika (CAF) ili itoe ufafanuzi kama suala la wao kushirikiana na EFF katika masuala ya uhamisho yanawezekana.


EFF iliingia matatani baada ya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo kumwondoa madarakani Rais wake Dr. Ashebir Woldegiorgis na kuweka uongozi mpya bila kufuata utaratibu. Julai 29 mwaka huu, FIFA iliifungia EFF kutokana na hatua yake hiyo.


Duh! Jamaa ana gundu?


2 comments:

MARTIN PAULO SINGANO said...

Hana gundu tayali kesha luhusiwa kucheza huko ethiopia st georige

familia yake yote kwa sasa inaishi huko
huku atakuja sababu ya maximo tu

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___