Saturday, October 18, 2008

Ligi Kuu ya Vodacom

18.10.2008
Toto Africa vs Simba ............... 4 - 1
Prisons vs Polisi Moro..... 1 - 1
Azam vs Kagera Sugar.............1 - 2
19.10.2008
Yanga vs Polisi Dom ..........3-1

30 comments:

Anonymous said...

vipi game la prison na polisi moro?

Anonymous said...

Nasikia mnyama kauliwa tena na vijana wetu...mida ya saa kumi nambili za bongo alikuwa kapigwa kimoja!!!! Kuna mwenye zaidi....

Marco
Canada

Anonymous said...

duh hii noma sasa itabidi tusiingie uwanjani tuwasaidie point.

Anonymous said...

Myama kauwawa bao 4-1 na Toto Africa.
Jamaa lazima wapigane duh.

Mzozaji
Dar

Anonymous said...

inasemekana mnyama anajiandaa kukimbia aibu nyingine tarehe 26.

Leo wamepewa kipigo ambacho hawajakipata kwenye ligi tangu 1990.

Anonymous said...

Kumbukeni mwaka jana Toto pia alimchapa mnyama 3-1 Kirumba, kwa hiyo mnyama ni teja ...

Anonymous said...

Turekebishe hizo takwimu, mwaka jana alichapwa 3-2,siyo 3-1 kwa hiyo alijitahidi kuliko mwaka huu.Hali hii mnyama atamaliza nyasi pia atakula nini baada ya hapo.Na yule mzee wa kupima maji sijui safari hii kama kijiti hakitazama.Yetu macho

Anonymous said...

1,2,........4 mmh!! yamekuwa mengi mno,huyu na villa wanatofauti gani.

Anonymous said...

Nimesikia jamaa mmoja kihojiwa Kirumba hali ya timu yao,alichosema ni kuwa alivyoiona timu imeoza kila sehemu,hivyo akawashauri viongozi wao nao wale kona siku ya tarehe 26/10 kwa kuwa anavyo iona yanga na kiwango chao kunaweza kutokea maafa makubwa uwanja mpya. Lakini hii inawezakuwa janja tu, sisi akiliyetu iwe palepale

Anonymous said...

mimi nadhani mechi ya yanga na simba hakuna tena sijui kama timu itarudi dar

Anonymous said...

ohhhhhhhhhhhhhhhh, mambo hayo

Anonymous said...

ni kujiandaa tu kikamilifu. mpira ni mpira tu! walimfunga kagera sugar ambayo ilitutoa kamasi!

Anonymous said...

... na sisi tulimfunga Azam aliyewatoka kamasi ...

Anonymous said...

Dakika 25 zimeondoka, ni 1 - 1.

Yanga ilipata bao lake dk ya kwanza kupitia kwa "Chuji"

Anonymous said...

Dakika ya 32, tumepata bao la pili. Mfungaji ni Jerry Tegete

Anonymous said...

nani yuko golini leo Kaseja?

Anonymous said...

Halftime, Yanga 2 Polisi 1

Anonymous said...

mimi ndo nadaka leo

Anonymous said...

wewe mdau wa Kuwait? unayedakia kwa nyuma ha ha ha

Anonymous said...

macho yetu ktk blog endelea kutupatia habati CM kazi nzuri

Anonymous said...

Dakika ya 70, Yanga 3 Polisi 1.

Boniface Ambani anapachika bao la 3.

Anonymous said...

Wajameni, huu msimu nafikiri ni wa mwisho kwa Mwaikimba, Yusufu Hamis na Mtiro kukipiga Yanga mnasemaje?

Anonymous said...

Mpira umekwisha kwa ushindi wa 3-1.

Kwa ushindi huu, Yanga imefikisha pt.24

Idadi ya magoli ya Ambani ni sawa na pointi za Simba!

Anonymous said...

Miaka yote huwa tunamkosa mnyama lakini tukimkosa mwaka huu tutakua sie wendawazimu, kwa sababu uwezo tunao, nia tunayo, mpira tunao, mshikamano tunao, mkwanja upo, morali kwa wachezaji na viongozi inaonekana ipo, sasa tukiwakosa tar.26 basi ni uzembe wetu.

Anonymous said...

mimi natabiri goli 5-0.naamini kabisa mpira wa yanga ,babu kubwa.

Anonymous said...

mimi natabiri goli 5-0.naamini kabisa mpira wa yanga ,babu kubwa.

Anonymous said...

mimi pia sielewi ni vipi mnyama atapona mwaka huu kama ni mpira wa uwanjani tu.Mnyama mpaka sasa hanatofauti na hizi timu tunazo funga 3, 4, 5. Wakitufunga tena basi hatutaweza kuwafunga tena milele.Kwa hali ya kikosi hiki,kikiwa safi kabisa siku hiyo mnyama akikaa vibaya hatausahau mwaka huu.

Anonymous said...

Mimi sitaki kusema chochote kuhusu mechi hiyo.Mpira wa Yanga na Simba ninacho jua mimi ni kwamba tunafungwa kisaikolojia wala si kwa sababu Simba huwa wametuzidi uwezo.Kwa kawaida huwa tunafungwa kabla hata mpira haujachezwa.Ikiwa wachezaji watajengwa vizuri kisaikolojia waione mechi hiyo ni kama hizi zote wanazo cheza sielewi ni kwa nini tusimfunge Simba. Hofu yangu ni hiyo.Maneno yao mengi yanatufanya wote tuchanganyikiwe na kushindwa kujiamini.Hii ni kuanzia wachezaji hata mashabiki.Tutaweza kuwafunga iwapo tu tutaondoa hofu hiyo.Bila hivyo sitashangaa hata kidogo iwapo Simba watashinda mechi ya jumapili.Ukiangalia hata sasa jinsi wanavyoongea kwa kujiamini juu ya mechi hiyo pamoja na madudu yote haya wanayofanya kwenye michezo mingine.NAWAOMBA WANAYANGA WOTE TUSHIKAMANE TUIPE SUPPORT TIMU YETU,WACHEZE KWA KUJIAMINI.

Anonymous said...

Jamani mimi nashukuru sana waandaaji wa blog hii kwani kwa sisi tulioko ughaibuni inatusaidia sana kupata matokeo na msimamo wa ligi, kwa mfano binafsi jana usiku ilinibidi nitumie kama nusu saa kukokotoa msimamo wa ligi ya bongo kwa kutumia matokeo ya kwenye magazeti ya mtandaoni kabla sijagundua hii blog leo asubuhi, kwa saa za New York. Naomba pia muwe mnatuwekea na picha za wachezaji wetu wa Yanga wakiwa wanashangweka kwa mabao yao au makipa wa timu pinzani wakiokota mpira nyavuni.

Anonymous said...

Jamani mimi nashukuru sana waandaaji wa blog hii kwani kwa sisi tulioko ughaibuni inatusaidia sana kupata matokeo na msimamo wa ligi, kwa mfano binafsi jana usiku ilinibidi nitumie kama nusu saa kukokotoa msimamo wa ligi ya bongo kwa kutumia matokeo ya kwenye magazeti ya mtandaoni kabla sijagundua hii blog leo asubuhi, kwa saa za New York. Naomba pia muwe mnatuwekea na picha za wachezaji wetu wa Yanga wakiwa wanashangweka kwa mabao yao au makipa wa timu pinzani wakiokota mpira nyavuni. YANGA DAIMA, NAKUMBUKA ENZI ZILE ZA YANGA UMOJA WA MATAIFA ZINAONEKANA KURUDI MSIMU HUU.