Tuesday, November 18, 2008

Buriani Mzee Ngozoma Matunda

Makamu wa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Mzee Rashid Ngozoma Matunda amefariki dunia leo mchana katika hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam kwa muda mfupi.


Mzee Matunda ambaye aliwahi kushika nafasi ya Uenyekiti wa klabu hiyo anatarajiwa kusafirishwa hapo kesho kuelekea Mkuyuni mkoani Morogoro kwa mazishi.

Miongoni mwa mambo ambayo Matunda atakumbukwa katika kipindi cha uongozi wake, Yanga ilifanikiwa kucheza katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998. Hata hivyo mwaka uliofuata aliondolewa madarakani kabla ya kurejea tena katika safu ya uongozi wa klabu hiyo mwaka jana akiwa kama Makamu wa Mwenyekiti hadi alipokutana na mauti.


Buriani Mzee Rashid Ngozoma Matunda.

3 comments:

Anonymous said...

poleni sana familia ya mzee matunda na wana jangwani wote
sio siri kifo
cha huyu mzee
ni pigo kwa yanga bwana alitoa na Bwana ametwaa Amen Mdau Cuba

Anonymous said...

mzee matunda atakumbukwa daima sababu ya kuleta umoja katika Yanga, tunamuomba mwenyezi Mungu amlipe kwa yale aliyeyafanya Ameen

Binda DSM

Anonymous said...

HATUTA MSAHAU WANA YANGA WOTE MZEE MATUNDA KWA UMMOJA WAKE NDANI YA YANGA