Sunday, November 02, 2008

Ligi Kuu ya Vodacom

Msimamo wa ligi


Huu ni msimamo wa ligi baada ya kukamilika kwa mzunguko wa kwanza.

Pamoja na Yanga kuongoza ligi hiyo, bado inaweza kukabiliwa na upinzani kutoka kwa Kagera Sugar ambayo inaonekana kuwa na ngome isiyopitika kirahisi, kwani imeruhusu mabao matano tu.


Prisons ya Mbeya ambayo itawakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ilianza ligi kwa kusuasua lakini inaonekana kuzinduka mwishoni lakini inaonekana kukosa umakini (consistency) kwani idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa inalingana.


Wazee wenzetu Simba bado wana kazi kubwa ya kufanya katika mzunguko wa pili kama wanataka kutwaa ubingwa wa bara. Tofauti ya pointi ambazo wameachwa na vinara wa ligi hiyo - Yanga ni 14. Hii inamaanisha kwamba Yanga inatakiwa ipoteze michezo 5 ili Simba waweze kuifikia.


Timu mbili ambazo zipo mkiani mwa ligi hiyo Villa Squad na Polisi Dodoma bado zina nafasi ya kuepukana na hatari ya kushuka daraja kwani safari bado ni ndefu.

Tusubiri mzunguko wa pili unaotarajiwa kuanza mwezi Februari mwakani.

5 comments:

Anonymous said...

CM asante mkubwa wetu kwa hii huduma ama kwa hakika wewe ni mdau halisi wa Yanga Uchaguzi ujao itabidi ugombee nafasi ya uenezi au waanzishe cheo kipya cha AFISA HABARI ndani ya Yanga ili upate nafasi ya uongozi. Naona watoto wetu wa Mwanza hawako pabaya sana kimsimamo ingawa wanatakiwa kukomaa mzunguko wa pili kwani kila timu itakamia na ile michezo michafu ya kuuza na kununua mechi huanzia hapo kwani kuna timu huwa zinataka kulazimisha ubingwa huku zingine zikitaka kukwepa kushuka daraja!!! Wadau wa Tanga waisaidie African Sports irudi kwenye ligi jamani yaani timu itapotea hivi hivi hiyo kama ilivyokua kwa lile matawi ya Simba ya Iringa LIPULI F.C na Mwanza; Pamba, FC.
Kwa wale mashabiki wa Yanga na Liverpool au Arsenal basi boleni sana kwani vigogo wote pua chini, Man United magoli kama handball au netball.teh teh

Anonymous said...

Kuna sababu gani za kuwa na ratiba ya ligi kama hii tuliyonayo? Mbona wakubwa wetu CAF ratiba yao ni ile ya zamani -Jan hadi Dec?

Ligi za ulaya huwa zinaanza Agosti hadi Mei kutokana na mazingira na hali ya hewa. Mwezi June/Julai wachezaji na viongozi huwa wanaenda likizo ya majira ya joto (summer).
Wakati mwingine June huwa yanafanyika mashindano ya kombe la bara la ulaya au dunia.

Baadhi ya ligi za ulaya mfano hispania huwa wana mapumziko ya wiki 3 December hadi Januari kwa sababu ya majira ya baridi (winter)

Sioni sababu ya sisi TZ kuwa na ratiba kama ya ulaya.

Hali ya hewa inaturuhusu kucheza februari hadi Decemba na mshindi kushiriki mashindano ya CAF/CECAFA mapema mwaka unaofuata. Pia michuano ya Afrika huwa inafanyika Jan au feb. Hali kadhalika Decemba/Januari ni muda mzuri kufanya usajiri kabla ya ligi kuanza. Ndio maana naupenda mfumo wa ratiba ya zamani kuliko ya sasa.

Sioni sababu pia ktk mfumo huu uliopo ni kwanini ligi isimame Novemba hadi Feb. wakati hali ya hewa inaruhusu michuano kuendelea.

Pia ligi yetu TZ huwa iko likizo kipindi cha Juni-Agosti kipindi ambacho wapenzi wa mpira huwa wamevuna mazao na kuyauza hivyo kibiashara. Michezo ingefaidika kimapato na wakulima (mashabiki) waliovuna na kuuza hasa maeneo ya Mwanza, Mbeya, Songea n.k.

Kwa kifupi naomba kujua haya mabadiliko ya ratiba yana manufaa gani kwa taifa na michezo?

Pia nashangaa kuona uwanja mpya wa Taifa uko 'idle' karibu kila mwaka hauna mechi au matukio yoyote. Huo uwanja unatakiwa uwe bize kuandaa michezo na matamasha mbalimbali ili kujiingizia kipato. Mi nadhani huo uwanja ulijengwa kwa fedha za misaada na mikopo yenye riba. Sasa deni la uwanja huo linalipwaje ikiwa umekaa wazi tu huku kuna watu wameajiliwa hapo na wanalipwa na deni lake linazidi kukua? Inabidi watanzania tuchangamke tutafute namna ya kujiingizia kipato maana huo uwanja tayari ni kitenga uchumi!

Kumbuka huo ni Uwanja wa Taifa usiwe Makumbusho ya Taifa! Wahusika tafuteni namna ya kuingiza fedha kwa kuutumia huo uwanja, sio sifa uwanja kukaa bure tu mwaka mzima wakati gharama za kuuendesha ziko palepale na wakati mwingine zinaongezeka!

Huo uwanja ni LAZIMA ujiendeshe kibiashara na sio kutegemea mgao toka bajeti za serikali au ikulu!

Anonymous said...

Tunashukuru kwa hoja zako nduguyetu.Mimi nitachangia hasa kwa upande wa musimu wa ligi. Mfumo huu mimi naona ni mzuri isipokuwa unatakiwa kuboreshwa. Naseme ni mzuri kwa sababu gani,ni kweli michuano mingi ya CAF inaanza januari na kuendelea,hili lilikuwa na athari sana kwa vilabu vyetu kwa sababu ndiyo kwanza wanamaliza usajili na mashindano makubwa yanaanza, kabla timu haijakaa vizuri mmesha tolewa, kwa sasa timu itaingia kwenye mashindano wakiwa tayari wanakikosi cha kwanza.Tuangalie mfano wa Yanga juzi kwenye mashindano ya kagame,tulicheza yale mashindano tukiwa hatuna kikosi cha kwanza.Mchezaji kama Mwalala hakucheza mechi hata moja.Lakini sasa tumeona kuwa combination ya Mwalala na Ambani ndiyo ya ushindi,tukatolewa mapema huku tukiwa na timu bora nafikiri kuliko zote.Magoli yaliyo mafungwa magolikipa wetu nadhani ingekuwa ni Obren hakuna goli pale. Lakini wakati ule nani alijua huyo mzungu ni kiwango.Matokeo yake tukatolewa mapema sana bila kutarajia.Naamini kwa sasa timuikiingia mashindano yoyote hatuendi kujaribu tena.
Kinachotakiwa kufanyika ni kwamba kusimama ligi muda mrefu hivi ni kutokana na uchache wa timu katika ligi.Inatakiwa kuwe walau timu 16 ilikuongeza kwanza ushindani pia kuongeza muda wa wachezaji kucheza tatu ni kuwa na wachezaji wengi katika ligi kuu.Tuna vijana wengi wazuri ambao hawacheji ligi kuu kwa sababu ya kukosa timu za kuchezea.Siyo sahihi nchi yenye watu wanaofikia milioni 40 kuwa na timu 12 tu katika ligi kuu.Ligi inakosa ushindani wa dhati.Ukiongeza timu 4 unaongeza wachezaji karibu 120,lakini pia mizunguko mingine kama nane hivi itaongezeka.
Kwa hiyo ninacho ona tatizo ni uchache wa timu,mpango wenyewe ni mzuri.

Anonymous said...

nakubaliana na Masebe. Mfumo huu mpya uanazipa timu zetu muda wa kusajili na kujiandaa kwa mashindano. Kinachotakiwa ni kuboreshwa.

Nadhani kipindi cha Nov - Feb ni kirefu mno, wachezaji wasipokuwa makini watashuka viwango sababu ya kukosa competition.

Nadhani huu mdio ungekuwa muda ma mashindano ya Afrika Mashariki na Kati, Tusker, Taifa cup etc.

Kwa Yanga napendekeza wautumie muda huu kujiandaa kwa ligi ya mabingwa mwakani.

Shukurani kwa mkuu CM kwa huduma.

Anonymous said...

Asante sana ndg Masebe na msomaji mwingine hapo juu kwa maelezo na ufafanuzi kuhusu mfumo/ratiba ya ligi.

Mimi ndie niliyeomba ushauri au ufafanuzi wa ratiba ya ligi. Kwa kweli maelezo yenu yamenipa mwanga wa kutosha kuhusu nini kinaendelea hapo nyumbani ktk medani ya soka.

Kimsingi nakubaliana nanyi kabisa.

Nami pia napenda kumshukuru na kumpongeza 'cm' kwa kutuwekea jukwaa la kubadilishana habari, mawazo na uzoefu! Wana-Yanga tunawasiliana moja kwa moja toka sehemu mbalimbali duniani kutokana na juhudi na ubunifu wa 'cm'.
Hongera sana 'cm' kwa kutuunganisha wana-Yanga!

M.R., United Kingdom