Friday, November 07, 2008

TFF yauma na kuipuliza Yanga
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la soka nchini (TFF) limetoa maamuzi mbalimbali kwa vilabu pamoja na wachezaji kwa makosa mbalimbali kufuatia kupitia ripoti za wasimamizi wa michezo kadhaa ya ligi kuu ya Vodacom.

Miongoni mwa maamuzi yaliyotolewa na TFF ni pamoja na kuipatia Yanga ushindi wa mezani wa pointi 3 na magoli 3 katika mechi zake mbili dhidi ya Polisi Morogoro na Polisi Dodoma.

Katika mechi zote hizo mbili, vilabu hivyo vya Polisi vimebainika kuchezesha wachezaji ambao walikuwa wanatakiwa kutumikia adhabu ya kufungiwa mechi moja baada ya kuonyeshwa kadi tatu za njano katika michezo yao iliyopita. Katika michezo hiyo Yanga iliifunga Polisi Dodoma 3-1 na mechi dhidi ya Polisi Morogoro iliisha kwa sare ya 0-0. Kwa maamuzi hayo, Yanga sasa imefikisha pointi 30.

Wakati huo huo, mshambuliaji Ben Mwalala amefungiwa mechi 3 na kutozwa faini ya 300,000/= baada ya kubainika kupigana uwanjani katika mechi dhidi ya Simba ambapo yeye na beki wa Simba - Meshack Abel walionyeshana ubabe. Abel naye amepewa adhabu kama hiyo.

Pia TFF imezitoza Yanga na Simba faini ya 300,000/= kila moja kufuatia mashabiki wa timu hizo kurusha chupa zenye vimiminika mbalimbali uwanjani katika mpambano huo. Aidha wachezaji Athumani Iddi na George Owino wa Yanga wamepewa onyo kali baada ya kamati hiyo kubaini matukio mbalimbali yasiyo ya kimichezo ambayo hayakuonwa na mwamuzi katika mchezo dhidi ya Simba uliopigwa mwishoni mwa mwezi uliopita.

6 comments:

Anonymous said...

Mechi ya 0-0 ni Polisi Moro siyo Poliso Dom. Mwalala anaanza kutumnikia kifungo kutokea mechi gani? Je, mechi ya mwisho wa ligi inahesabika?

Anonymous said...

mdau hapo juu tumepata ushindi wa chee mechi zote mbili bila kukata rufaa hata hao polisi Dom pamoja na kuwafunga walichezesha mchezaji mwenye kadi so kale kagoli kao kamoja wamekapoteza si unakumbuka matokeo yalikua 3-1? sasa 3-0

Anonymous said...

Magoli pia yatakuwa ni 2 na siyo 3.Kwa hiyo itakuwa 2-0.Nafikiri Mwalala adhabu yake ni kuanzia mechi ile iliyopita kwa sababu nayo hakucheza kwa ajili ya hiyo kadi.Hizo 300,000 tumetozwa za nini,timu yetu ilishiriki uchawi pia?

CM said...

Mdau wa kwanza nashukuru kwa kunirekebisha. Ni kweli niliandika Polisi Dodoma badala ya Polisi Morogoro. Tayari nimerekebisha.

Anonymous said...

Naunga mkono maamuzi ya TFF. Kwa kweli hapo wamefanya kazi kitaaluma.
Timu, wanamichezo na mashabibiki tujifunze kuheshimu taratibu za michezo na vyombo vinavyosimamia michezo viheshimiwe pia.

MR, England

Anonymous said...

Jamani lazima klabu imlipie mwalala alitupa raha na kama klabu haiwezi basi tualifiwe wapenzi na wanachama tumlipie hivyo vijisenti.
Masebe, magori siku hizi ni 3 siyo 2 kama zamani.