Thursday, February 12, 2009

Yanga sasa kuondoka leo

KIKOSI cha wachezaji 21 wa Yanga, viongozi sita kinaondoka leo jioni kuelekea Comoro kwa ajili ya mechi ya marudiano na Etoile d'Or Mirontsy itakayochezwa Jumapili kisiwani humo.

Awali Yanga ilipanga kuondoka Jumamosi kwa usafiri wa Shirika la ndege la Comoro (Air Comoro), lakini uongozi wa klabu hiyo umeamua kuondoka mapema zaidi kwa ndege ya Kenya Airways (KQ) kwa vile "lolote linaweza kutokea" endapo watatumia usafiri unaomilikiwa na nchi ambayo wanakwenda kupambana nayo.

Msafara huo utaongozwa na mjumbe wa kamati ya utendaji wa TFF ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha soka la wanawake TWFA - Lina Madina Mhando.

Wachezaji watakaoondoka leo ni Obren Curkovic, Shadrack Nsajigwa, Amir Maftah, Wisdom Ndhlovu, Nadir Haroub ( Cannavaro), Godfrey Bonny, Mrisho Ngassa, Athuman Idd ( Chuji) na Boniface Ambani.
Wengine ni Jerry Tegete, Kigi Makasi, Juma Kaseja, Fred Mbuna, Shamte Ally, Nurdin Bakari, Vicent Banabas, Abdi Kassim, Ben Mwalala, Mike Barasa, Abuu Mtiro na Castory Mumbala.

Timu hiyo itarejea nchini Jumanne ijayo.

7 comments:

Anonymous said...

Jamani. Timu imeondoka?

Anonymous said...

Timu iliondoka jana huku ikimwacha Athuman Iddi ambaye ni majeruhi.

Anonymous said...

Wakati mwingine tunawalaumu TFF lakini CAF nao wana mambo ya ajabu kabisa. Kama taifa stars itacheza fainali basi tutakuwa na siku tatu za kujiandaa na wamisri. Kwa ushauri wangu wachezaji watakaobaki waandaliwe kwa ajiri ya mechi hiyo kwa maana itakuwa ngumu kuwaunganisha na wengine.

Anonymous said...

Timu ya Taifa itatolewa mapema sana kwenye raundi ya kwanza.Hivyo tusijali tutakuwa na muda wa kujiandaa.

Anonymous said...

Wamisri hawaendi kwenye haya mashindano wanajiandaa hata tukitolewa mapema mechi ya mwisho ni tarehe 28 na fainali ni tarehe 3 na mechi na wamisri ni 13-15 March. Hebu niambie hapo tutakuwa na muda gani wa kujiandaa na timu kali kama ya wamisri lazima mikakati ianze mapema.

Anonymous said...

Jamani hivi hawatakiwi kucheza leo?

Anonymous said...

vipi kuna matokeo yoyte ya game yetu na wacomoro?
mdau-uk