Tuesday, March 17, 2009

Cheki magoli ya Al Ahly

Ndugu mdau hebu cheki magoli tuliyofungwa na Al Ahly kwa kugonga hapa.

5 comments:

Anonymous said...

upande wa ulinzi wa kushoto vipi?

Anonymous said...

ni mistake za kawaida ndogo tu,magoli yote yanaonyesha kuwa na sura moja ktk kufungwa,

nikuwa hata huyo mpigaji cross alipiga cross,lakini baada ya kipa kupangua ni kuwa jamaa mabeki wakati walimuwacha peke yake,jamaa aliechomekewa pia beki hawakumkaba alikuwa peke yake,goli la 3 beki walimuwachia peke yake mfungaji nadhani wakidhani ofside lakini,ni makosa ambayo team kubwa duniani zinafanya same mistakes,
kwahio sio mbaya kufungwa ukajifunza, ila inabidi coach aone makosa ya defenders wake.

ERNEST B. MAKULILO said...

Habari zaidi!
Yanga basi tena-Kondic
Abdallah Msuya, Cairo
Daily News; Monday,March 16, 2009 @21:15

Habari nyingine
Abdulhalim naye awekwa kikaangoni Maisha Plus
Copa Coca-Cola kutumia mil 450/-
Jalada la Mwintanga halipo mahakamani
Pan Africa kuchaguana Aprili 12
Wachezaji Yanga wadai kuhujumiwa
Maximo awashukia makocha wazawa
Yanga basi tena-Kondic
Mgosi, Boban waipaisha Simba
Maximo sasa wa hapahapa
Kova kushughulikia wizi wa mapato

Kocha Mkuu wa Yanga, Dusan Kondic amepoteza matumaini ya kufika hatua ya pili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya timu yake kuchapwa mabao 3-0 na mabingwa wa Afrika Al Ahly katika mechi ya awali ya raundi ya kwanza juzi.

Akizungumza na 'HabariLeo' mjini hapa, Kondic alisema tofauti ya kiwango cha timu hizo mbili ni kubwa, hivyo timu ya Tanzania itakuwa ni vigumu kupita mbele ya timu bora ya Afrika.

“Wana wachezaji wazuri. Wana mchezaji Aboutrika (Mohammed), ambaye ni mchezaji mzuri wa Afrika ambaye alipendekezwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, pia wana Barakat ambaye pia ni mchezaji mzuri, sisi hatuna wachezaji wenye viwango kama hivyo,” alisema Kondic.

“Sikuja Yanga kunyakua ubingwa wa Afrika kwa mwaka huu, bado tunajenga timu, imani yangu tunaweza kuwa bora mwakani. Tumekutana na timu imara sana katika raundi ya kwanza, labda mwakani, nafasi nyingine itatujia tutacheza na timu ambayo ina kiwango cha chini ukilinganisha na Ahly.

“Jambo la msingi ni kuwa tunaweza kushinda ubingwa wa ligi msimu huu, jambo ambalo litatupa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.” Pia Kondic amemtetea kwa nguvu kipa wake Obren Curkovic ambaye analaumiwa kwa bao la pili kuwa amefungwa kizembe.

“Watu wanazungumzia kosa moja alilofanya, lakini wamesahau jinsi alivyookoa hatari nyingine. Huenda mabao ya kufungwa yangekuwa mengi kuliko hivi sasa, huenda zingefika hata mabao sita, kama si juhudi za kipa kuokoa.” Pamoja na kudai wapinzani wake ni bora, Kondic amewasifia wachezaji wake hasa Nurdin Bakari.

“Tulicheza vizuri sana kwenye robo ya mwisho na kufanikiwa kuwapa shinikizo wapinzani wetu, lakini hatukuwa na bahati ya kupata hata bao moja ambalo lingetupa manufaa wakati wa mechi ya marudiano. “Nurdin (Bakari) aligonga mwamba na alistahili kuwa mchezaji bora wa mechi kutokana na kiwango alichoonyesha,” alisema Kondic.

Mserbia huyo pia amemlalamikia mwamuzi kwa kushindwa kuizawadia timu yake penalti baada ya mchezaji wa Ahly kushika mpira kwenye eneo la hatari. Lakini baadhi ya mashabiki walioambatana na Yanga, mjini hapa wamemtuhumu Mserbia huyo kwa kuchangia kufungwa timu yao kutokana na uteuzi wa wachezaji.

Baadhi ya mashabiki walipendekeza kipa awe Juma Kaseja badala ya Obren, na pia kuhoji uamuzi wa kumuacha George Owino na kumuingiza wakati timu imeshapoteza mechi. Alipoulizwa kuhusu uamuzi wake wa kumuacha benchi Owino, Kondic alisema alikuwa sahihi kuanza na kiungo mzuiaji Godfrey Bonny badala ya mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Kenya kwani ilikuwa ni moja ya mipango yake.

Baadhi ya wachezaji pia wameelezea kutofurahishwa na mbinu za ufundishaji za Kondic na kutaka kuwapo na mazoezi ya nguvu na mechi za kirafiki kwa ajili ya mechi ya marudiano. Yanga inatarajia kuwasili leo asubuhi na inatarajia kucheza na Toto African kwenye mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara keshokutwa na Polisi Moro.

Naye Mwandishi Wetu anaripoti kuwa, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodger Tenga amesema ana imani kuwa Yanga ina uwezo wa kuishinda Al Ahly pamoja na kipigo cha Jumapili cha mabao 3-0. “Inahuzunisha kuona wawakilishi wetu kwenye michuano mikubwa wamefungwa kwa mabao mengi, lakini katika soka lolote linaweza kutokea. Ninashawishika kuamini Yanga wana uwezo wa kufanya vizuri katika mechi ya marudiano, hasa ukichukulia kuwa watakuwa wakicheza uwanja wa nyumbani.” Tenga amemtaka Kondic kutokata tamaa, badala yake ni kubainisha makosa yaliyojitokeza na kuyafanyia kazi kabla ya mechi ya marudiano.

Anonymous said...

vipi game ya leo huko matokeo?

Unknown said...

We do not need to blame Obren for this,look at the first goal,no defender was picking up the striker he was left alone,he was totally unmarked,he controlled the freely,the second very good exchange passes found the striker unmarked,where was the defender to harras him, it is very obvious that the left side of defender is a problem,it was totally poor marking.Quite a suprise the club of great defenders,the likes of Nsajigwa,Nadir,Wisdom allowing easy goals like this ahhh! horrible, they actually need to work hard,as a Young African fan,I know they can do wonder in the second leg,but confidence is really important in the second leg tie,if we have good difence,with the striking force we have,Ambani,Ngasa,Mwalala and midfielders like Chuji,Nurdin,Babi,they can do a wonderful job.