Tuesday, March 24, 2009

Yanga kutwaa Ubingwa leo?

YANGA inahitaji pointi tatu za mpambano wake leo dhidi ya Toto African utakaofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ili iweze kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Kwa maana nyingine, timu hiyo ambayo kwa sasa ina pointi 43 inaongoza kwenye msimamo wa ligi na itafikisha pointi 46 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine.

Awali, timu hiyo ilikuwa na pointi 45, lakini habari ambazo zimepatikana jana zilieleza kuwa pointi mbili za chee ilizokuwa imepewa awali na Shirikisho la Soka Tanzania TFF kutokana na Polisi Morogoro kubainika kuchezesha mchezo asiyekuwa na sifa, zimekatwa karibuni na hivyo timu hiyo kubakia na pointi zake 43.

Hata hivyo, habari zilieleza kuwa Polisi walikata rufaa na kushinda na kurejesha pointi yao na kuifanya Yanga ambayo imeshinda ubingwa mara nyingi kuliko wapinzani wao, Simba kutakiwa leo kuweka rekodi ya kuchukua ubingwa huo mara 22 kwa ushindi.

Mbali na kutwaa ubingwa huo, vijana hao wa Mtaa wa Jangwani na Twiga watakuwa wamejihakikishia nafasi nyingine ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya klabu bingwa Afrika mwakani.

9 comments:

Anonymous said...

Wadau Wenzangu
Mechi Mwanza inaendelea
Yanga 2 Total 1 hadi sasa.
Wafungaji Yanga ni Kaseja na Mike Baraza.
Nurdin Kakosa penalty
Ila uwanja una maji sana so mpira wa ufundi hauchezwi sana.

Anonymous said...

Tunaomba matokeo wadau mnaofuatilia mtanange!

Anonymous said...

Mechi ni half time. Matokeo bado kama ilivyo hapo juu

Anonymous said...

Mpira umekwisha matokeo Yanga 2 Toto 1. We are the champion once again

Anonymous said...

hureeeeeeeee,sasa hivi tunawezachezesha kikosi cha tatu sasa!

Anonymous said...

Kazi imeisha sasa, haya tungoje waarabu. Jamani nyinyi mliopo nyumbani, Jengo la Yanga limekwisha au bado? Vipi Uwanja umeanza kujengwa?

Nalitolela, P. S. said...

Pongezi kwa timu na kwa wanayanga wenzangu popote pale mlipo!

MARTIN said...

NAPENDA KUTOA HONGELA KWA VIONGOZI WOTE WA YANGA NA WACHEZAJI WOTE WA YANGA NA MASHABIKI WOTE WA YANGA KWA UBINGWA WA MAPEMA MNO MIMI MWANAYANGA MWENZENU JINA LANGU NI MARTIN PAULO SINGANO NAPATIKANA TANGA MJINI WAWEZA KUNIPATA PIA KWA NAMBA HII 0713-064-180 NASEMA KWAMBA TUKAZE BUTI HIVYOHIVYO NA HAWA WAARABU TUNAWATOA TUU WANAFUNGIKA TU SITUMEONA MAGORI YAHO BWANA WALA SI YAKUTISHA

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___