Wednesday, April 08, 2009

Obren atimkia Austria

Kipa mzungu wa klabu ya Yanga, Obren Circkovic ameondoka nchini kuelekea Austria kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini humo.


Hata hivyo Obren ameondoka huku akielezea kusikitishwa kwake na tuhuma anazoendelea kuandamwa nazo kwamba alipokea fedha ili acheze chini ya kiwango katika mechi dhidi ya Al Ahly huko Cairo ambapo aliruhusu nyavu kutikiswa mara tatu.


Akiongea katika mahojiano maalum na TBC, Obren alishangazwa na tuhuma hizo na amewaambia wanaomtuhumu kwamba amekuja nchini kucheza soka akiwa kama mchezaji professional hivyo anacheza mechi zote kwa bidii kubwa uwanjani. Aidha ameongeza kwamba anasikitishwa na ujumbe wa vitisho anaopokea mara kwa mara kwa SMS. "Siwezi kulazimisha watu waamini au wasiniamini, mimi nimekuja Yanga kufanya kazi na hadi sasa nimeifanya kwa moyo mmoja".


Ikumbukwe kwamba Obren ndiye aliyeiokoa Yanga katika mechi ya kwanza dhidi ya Simba msimu huu ambapo kama si uhodari wake tungeendelea na ule uteja wetu.


Hii si mara ya kwanza kwa Yanga kuwatuhumu makipa wake kuuza mechi mara baada ya kupoteza mechi muhimu. Makipa Sahau Kambi, Stephen Nemes, Juma Nkongo, Noel Pompi na Ivo Mapunda nao waliwahi kuhusishwa na tuhuma kama hizo ambazo wote walizikanusha.


Yanga sasa imebakiwa na makipa wawili Juma Kaseja na Stephen Marashi. Awali Kipa Ivo Mapunda aliuzwa kwa klabu ya St. George ya Ethiopia.


6 comments:

Anonymous said...

jamani vipi fununu za usajili

Anonymous said...

huyu mchezaji akipata timu tu basi yanga wamngángánie walipe hela nzuri,isiwe kakimbia tu na kubakia kumuwachia kama walivyozowea makocha wa yanga na simba kukimbia bila kumaliza mkataba,kama ni huku ulaya unalipa hela ya watu yote ambayo ulitakiwa uitumikie kwa muda ambao ungelikuwepo na timu,pia kama umekatisha mkataba basi unatakia umpatie hela yake pia sio kuondoka tu,hata hao akina naider dos santos na yule aliekimbilia ethiopia kama mukianzisha esi hivi sasa kupitaia kwa fifa basi watakulipeni hela kibao,wenzetu wanaanzisha kesi hata kama ni za mwaka 1980 au zaidi kama kweli ulibainika na kosa hilo huko nyuma unawajibishwa tu,huyu akikimbia tu abanwe,mukija huku kwao hao jamaa hawaoni huruma na nyinyi,

Anonymous said...

Mzee hapo juu, huyu mchezaji hajakimbia, ameenda majaribio na kama atafuzu majaribio basi Yanga watalipwa gharama, Manji yupo makini sana kwenye hili, ndiyo sababu anataka masuala ya wachezaji yashughulikiwe na kocha pamoja na Madega. Kama hujui hili, basi wachezaji wafuatao wataondoka soon: Jerry Tegete (Vancouver Canada), Shadrack (Vancouver), Ambani (China), Athumani Idd (Uturuki), Ngassa (Majaribio - England), Nurdin Bakari (DC -United in USA), huyo golikipa (Austria), Boniface Bonny (Bosnia), Cannavaro (Bosnia), haya ningependa ujue juu ya hili pia, Yanga hawabahitishi, shukrani za pekee ni kocha wetu, ingawa baadhi ya watu wanampiga vita, lakini ndiyo kwa kiasi kikubwa anafanyikisha safari ya wachezaji hawa.

Jimmy

Austria

Anonymous said...

Hello Jimmy, vipi za Austria, wewe bwana na Yanga, vipi Dar lini? mimi nitakuwa Dar tarehe 13 May, vipi masomo mshikaji? naomba namba ya Tegete basi, take care,

Mussa,

China

John Mwaipopo said...

Hapa washabiki tunakosea. Haifai kumshutumu kipa kama huyu. Tumezidi sana kudhani tunahujumiwa. Pale hata angekuwa Oliver Khan Kichapo kilikuwepo tu.

Anonymous said...

Wana yanga tuweni makini hili ni zengwe la simba ili kufanikisha mambo yao april 12 na sasa wamemgeukia kocha nasikia wanamtishia kwa kisingizio ni mashabiki wa yanga. Uongozi , wanachama na washabiki tuwe makini maana jamaa misheni yao imeshakamilika kazi kwetu