Sunday, August 16, 2009

Mtibwa yatwaa Ngao ya Hisani

Mtibwa Sugar imetwaa Ngao ya hisani kwa kuifunga Yanga kwa 2-1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Uhuru.

Bao la ushindi la Mtibwa Sugar lilipatikana katika dakika za majeruhi (90+2) baada ya timu hizo kutoshana nguvu ya 1-1 huku bao la Yanga likifungwa na Mike Baraza.

Mchezo huo wa ngao ya hisani ni kuashiria ufunguzi wa msimu wa ligi kuu ya Vodacom 2009/10 unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki ijayo.

8 comments:

Anonymous said...

Sasa huu usajiri wa mbwembwe nini tena?

Anonymous said...

Wadau hii timu mliona ilivyofanya mazoezi kwa ubabaishaji. Maandalizi so far si mazuri. Wachezaji wa kigeni hawakuripoti mapema (kutokana na kuchelewa kwa makubaliano, nk) na wachezaji wengine hawakulipwa mishahara ya miezi kadhaa. Hivyo mazoezi ya mapema hayakuwepo kabisa. Kama haturekebishi mapema, mwaka huu unaweza usiwe wetu ingawa timu ina nyota na damu changa yakutosha.

Mara zote tunasahau sana namna ya kujiandaa. Viongozi wajipange vyema kumpa nafasi kocha ili timu ikishindwa sisi wadau tumlaumu kocha. Kwa sasa Kondic hana kosa kabisa. Macho yetu yawe kwa viongozi. Kwa ujumla hadi sasa timu haijawa moja. Ni shaghala baghala. Tunahitaji umakini hapa.

Mdau Yanga
Mannheim, Germany

Anonymous said...

Mdau kutoka Manheim, Germany
Tumekusikia, haya yetu macho sasa vipi kale ka mradi ka web site kamfikia wapi?

Anonymous said...

Yanga kufungwa jana sio mwisho wa ligi tulieni na hii blog iwe inaweka mambo mengi mapema kuna wanachama wengine hawasomi magazeti mara kwa mara kwa kutegemea blog hii

Anonymous said...

Hii ni asante ya kumtegemea mtu mmoja yaani Manji, viongozi wetu hawana mipango mbadala ya kusaka hela ndo maana hawakuweza kuwalipa wachezaji kwa wakati na mazoezi yakaanza kusuasua.

hawa akina madega na wenzake hawatutakii mema mimi nashauri wasichaguliwe tena awamu ijayo.

halafu huyu mchezaji kutoka Cameroon ivi kocha alimfanyia utafiti kabla ya kumsajili?

yaani nimemwangalia kwenye mechi mbili zilizopirta ni ghalasa hakuna mfano.
kama kuna mchezaji anatakiwa kuachwa basiwa kwanza awe huyo kwani is the next Mwaikimba.

bora hata tuiache nafasi moja kwa ajili ya dirisha dogo kuliko kuendelea na hili jibaba.

msimu huu una kila dalili za kufulia kwa timu yetu, wenzetu wamejiandaa tusipoangalia tutapigwa bao saaana.

tusijeanza kulaumiana

nawasilisha lakini napendekeza pia aajiliwe kocha wa kuwajenga wachezaji kistamina, wachezaji wetu wazito sidhani kama wiki moja ilobaki itatosha kurekebisha kasoro kwani ni nyingi mnoooooooo.

Anonymous said...

Dear Mdau hapo juu,
Kale ka-mradi ketu ka-web kako vizuri tu. Domain tumeshalipia na kuregister na first layout iko tayari. Tuko kwenye ku-finalize layout na components as well as data collection.Angalieni www.yangasc.com ila hamtapata access ya kuona layout na components kwani iko under administrator access kwa kuwa inafanyiwa kazi. Ni wale tu walio kwenye hii project ndio wana full access ya stage nzima.

Labda tu ningewaomba wadau wengi information/taarifa/pictures nk vya Yanga ya miaka yote tokea kuanzishwa kwake 1935 wanitumie kupitia geoffrey.mwambe@gmail.com.

Otherwise, tutapeana taarifa mwishoni mwa mwezi wa 10, na tentative date ya launching is December 2009. Hatutarajii kukwama ili tuweze ku-meet deadline tuliyojiwekea ingawa ya Mungu ni mengi na pia maisha binafsi yanatusubiri. Naamini wadau mtaifurahia website ya Yanga.

Hongera mdau uliyekumbusha kwa kuwa na kumbukumbu nzuri juu ya web.

Mdau Geoff Mwambe

Mwanafyale,

Nimeona hongera saana kazi inaonekana inakwenda ingawa sijaruhusiwa kuingia ndani