Sunday, August 23, 2009

Mwalusako, Sendeu, Mweje waajiriwa wapya Jangwani

Katika kutekeleza agizo la TFF la kuwavitaka vilabu vyote vya Ligi Kuu kuwa na watendaji wa kuajiriwa, klabu ya Yanga imewatangaza watendaji hao.

Mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Lawrence Mwalusako sasa anakuwa Katibu Mtendaji mpya, Mwandishi wa TBC Luis Sendeu anakuwa Msemaji wa klabu ilihali Mweka Hazina Msaidizi wa Uongozi wa sasa Geodfrey Mweje anakuwa Mhazini wa klabu.

.................Njoroge atemwa

Beki wa kimataifa wa Yanga kutoka Kenya John Njoroge ametemwa na klabu ya Yanga ili kutoa nafasi kwa George Owino ambaye amerejeshwa klabuni hapo na TFF.

Kuondolewa kwa Njoroge sasa kunaifanya Yanga kuwa na wachezaji 10 ambayo ndiyo idadi ya mwisho ya wachezaji wa kigeni inayotakiwa na kanuni za TFF.

Sababu kubwa za kuondolewa kwa Njoroge ni kutokana na kuitwa kwake mara kwa mara na kikosi cha timu yake ya Taifa ya Harambee Stars na hivyo atakuwa na muda mdogo wa kuitumikia klabu hiyo katika nusu ya kwanza ya ligi kuu ya Vodacom.

Hata hivyo Yanga itakuwa ikimlipa mshahara pamoja na kumtumia katika mechi za kirafiki ili kumweka katika kiwango kizuri ili aweze kusajiliwa katika dirisha dogo litakalofunguliwa mwishoni mwa mwaka.

No comments: