Thursday, September 17, 2009

Chuji aongezewa adhabu

SIKU moja baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kukata rufani Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, kupinga kufungiwa kwa kiungo wake, Athuman Idd Chuji, shirikisho hilo limemfungia miezi mitatu tena kwa kile kilichoelezwa kukithiri kwa utovu wa nidhamu.

Kwa mujibu wa Kamati ya mashindano ya TFF, imemwongezea adhabu ya miezi mitatu kuanzia jana kwa kile kilichoelezwa kuonyesha utovu wa nidhamu katika mchezo wa Septemba 5 dhidi ya Majimaji ya Songea kwa kuwaongoza wachezaji wenzake wa Yanga kufanya fujo na kumzonga mwamuzi baada ya mchezo.

Chuji ambaye awali alipewa adhabu ya kutocheza kwa miezi mitatu tangu Septemba 6 baada ya kamati kukaa imemwongezea adhabu ya miezi mitatu tena na kulipa faini ya Sh500,000 kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu.

Adhabu hizo zinakwenda sambamba na sasa ataongeza siku 11 katika adhabu ya awali ya miezi mitatu iliyokuwa inamalizika Desemba 16.

Kamati hiyo ambayo pia ilipitia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na wachezaji wawili wa klabu hiyo ambao ni kipa Obren Curcovic na Marashi Steven ambao walionyesha utovu wa nidhamu kwa kukataa kuheshimu maamuzi ya waamuzi, hivyo kwenda kuwazonga wakati Marashi akitokea benchi. TFF imeagiza Marashi apewe onyo kali kwa kuzozana na mwamuzi.

SOURCE: MWANANCHI

10 comments:

Anonymous said...

it is high time tumsaidie huyu kijana kwa faida yake

Anonymous said...

Ni vyema ytukaanza kuizungumzia mechi ijayo dhidi ya Mtibwa,
Nilihudhuria mechi iliyopita tulipotoka sare na JKT RUVU, katika mchezo ule tulizidiwa sana seheme ya kiungo, kwa kuwa tulimtumia Abdi Kassim ambaye hakuwa sawasawa kwani wenzetu walitawala sehemu hiyo.
pengine katika kuboresha ingefaa sehemu hiyo iboreshwe kwani Mtibwa nao si wabaya.
pia kuna udhaifu wa safu yetu ya ushambuliaji kutokaa na mipira, imefika mahali huwezi kumwona beki wetu amepanda kusaidia mashambulizi kwani kila mara wanakuwa na kazi ya kuokoa, nasikia Nsajigwa majeruhi,lakini siyo mbaya mnyalukolo Mbuna ataziba nafasi yake

Anonymous said...

Ligi bado mzee hapo juu. Ni kweli hatuchezi kitimu kabisa, lakini kuanzia mechi ya Mtibwa nadhani muziki utapigwa, kiuongo kutakuwa na Mganda, wazee ligi tunaanza Jumamosi... tumefika Moro.

JT

Anonymous said...

Hivi hawa viongozi wa TFF wanajua wanalolifanya au wanataka kukomona tu?? umeona wapi mchezaji anafungiwa miezi mitatu eti kwa sababu ya utovu wa nidhamu uwanjani?? Tafuteni records popote pale duniani kama kuna mchezaji ameshawahi kufungiwa miezi mitatu kwa utovu wa nidhamu uwanjani hivi nyie TFF mbona njama zenu ni kali sana?? Tunajua wazi kua mnampango wa kuwatengenezea Simba mazingira mazuri ili wawezekuchukua ubingwa maana hata mienendo yenu ni ya ajabu kwa kweli. Hebu angalia hili:- Yanga ilipotoka songea ikaja kucheza an Jkt Ruvu angalieni uchovu huo wa safari alafu Simba mmewapa muda mreefu wa kupumzika ili waje wacheze na toto african ya mwanza, mkaona haiyoshi mmewachezesha Manyema juzi alafu hao simba mmewaacha wajiandae ili wacheze na manyema jumamosi hii kweli haya si mazingira ya kuwapa simba ubingwa??

Hebu jifunzeni kwa wenzenu sasa mliona Drogba alichofanya wakati wa mchezo kati ya Barcelona na Chelsea, ulimwengu wote ulishuhudia alichofanya Drogba lakini adhabu ikatoka kafungiwa mechi tatu tu, Haya hapa juzi tu mmeona Adebayo alichofanya, kafunga goli kaenda kwa mashabiki wa arsenal naye kawa burned kwa mechi tatu tu how come nyinyi mumfungie mchezaji miezi sita?? kama mnataka soka la Tanzania likue basi acheni uonevu usiokuwa na msingi kwa wachezaji.
Naamini kabia kama Tenga unatembelea hum jamvini na ujumbe huu utakufikia.

Willy Udsm

Anonymous said...

acheni kulalamika...hizi ndizo mbinu mlizotumia miakia miwili iliyopita na mlisherekea sana..sasa mwaka huu hizo hizo mbinu zina watia kiwewe....hahahah..what goes around comes around...

Anonymous said...

Willy mbona unalalamika kama mbwa anayetaka kuzaa!!! Fujo afanye Chuji, halafu mnadai ni mbinu za kuibeba Simba. kwani hii ni mara yake ya kwanza kuonesha utovu wa nidhamu?? Mbona mnakuwa mnatetea ujinga? Ndio maana mpira wa Tanzania hauendelei maana kama mashabiki ndio akina Willy, hasara tupu. Mbona kuna wachezaji msimu uliopita walifungiwa kwa utovu wa nidhamu hukulalamika? au kwa vila hawakuwa wa Yebo Yebo? Kila nchi ina sheria zake kwa hiyo usilinganishe ligi yetu na za majuu. Tengenezeni timu yenu acheni bla bla hapa jamvini. Tunawasubiri kwa hamu sana na safari hii cha moto mtakiona

Anonymous said...

Willy, umeangalia ratiba nzima ya ligi kabla ya kuanza kulalamika hapa kuwa Yanga inaonewa? Ukiangalia vizuri utaona kuwa huko mbele Simba itakuwa na muda mfupi wa kupumzika between game zake. Acheni unazi wa kijinga!!!!!

John kpt said...

Willy uko sawa kabisa TFF inatakiwa kurekebisha sheria zake si sahihi kumfungia mchezaji miezi sita huku wakijua soka ndo ajira yake.
TFF wenyewe wanaona marefa wetu wanavyoboronga. Kwa maana hiyo marefa ndo wanaosababisha wachezaji kupatwa na jazba.
Halafu nyie mnaomshambulia Willy mmetokea wapi! Hili jamvi la wana jangwani nyie tengenezeni yenu msituletee lugha za kipuuzi hapa. Haiwahusu fuateni mambo yenu.

Anonymous said...

Wazee wa Msimbazi naomba niwaulize msimu uliopita mulisema wachezaji wa yanga wanatumia dawa za kuongeza nguvu ndio maana walikuwa wanashinda je msimu huu ina maana wachezaji wenu wanatumia dawa za kuongeza nguvu?

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___