Saturday, September 19, 2009

Dar mpaka Moro
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwPrIvhiE1AaZqpEI0NnIQAefzuBt-6wWZKQV7V_d0TaXElk9Vb7za7XTONxz2A2xtOdOLxP7KLF4XMtBsU8AXHCXiLOKxtLmg_77q81D4UwU40CoeiSbV0LMy-gpamlUxHZvSnA/s320/mtibwa+logo.jpg
Yanga leo inafunga safari mpaka Moro kupambana na Mtibwa Suga katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaopigwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini humo.

Timu zote mbili zinaingia katika mchezo huo zikiwa na kumbukumbu isiyoridhisha katika michezo yao ya mwisho ya ligi. Yanga ililazimishwa sare ya 2-2 na JKT Ruvu nyumbani wakati Mtibwa Sugar ililala kwa 1-0 kwa Majimaji huko Songea.

Yanga leo itamkosa beki wake wa kulia Shadrack Nsajigwa lakini itawakaribisha kwa mara ya kwanza msimu huu Mganda Steven Bengo na beki aliyerejeshwa na TFF George Owino kutoka Kenya.

Mechi nyingine ya ligi hiyo itapigwa katika uwanja wa Uhuru kwa Simba kupambana na Manyema Rangers.

17 comments:

Anonymous said...

Kazi imeanza Morogoro, mambo bado

Anonymous said...

bado matokeo ya mwanzo ngoma vipi huko nyumbani?

CM said...

dakika 50
MTIBWA 0 YANGA 0
MANYEMA 0 SIMBA 2

CM said...

DAKIKA YA 57:

YANGA imepata bao kupitia kwa Amir Maftah ikiwa ni dakika chache baada ya Yusuf Manji kufika uwanjani.

Mtibwa 0 Yanga 1

Anonymous said...

:)

CM said...

Dakika ya 60

Mrisho Ngassa anaipatia Yanga bao la pili.

Ni 0-2.

CM said...

dakika ya 65

Mtibwwa 1 Yanga 2

Anonymous said...

nawatakia kila la kheri iwe ndiyo mwanzo wa ligi

Anonymous said...

asante CM na update zako.naona ushindi upo tu.manji uwanjani timu itakuwa na morali

Anonymous said...

Du! Yaani timu bila Manji uwanjani hakuna ushindi??? Kaaazi kweli

Anonymous said...

wewe acha fitina hutakiwi hapa.

CM said...

Uwanja wa Uhuru Dar mpira umekwisha kwa ushindi wa 2-0 kwa Simba

Anonymous said...

huyo ni mnyama hutakiwi humu sisi ndio kwala kaka sema utakavyo sema shughuli ndo imeanza lete mambo CM mdau buruda!!!!!!!!!!!!

CM said...

Mpira umekwisha huko Moro kwa ushindi wa Yanga wa 2-1.

Kwa ushindi huo, Yanga sasa ipo katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi.

Eid njema.

Anonymous said...

Asante CM,ebwana kazi nzuri sanaaaa!!!
Eid njema na wewe mwana!

Anonymous said...

jamani kulikon Obrin mwaka huu kila mechi anatunguliwa au ndo kaseja keshamaliza kazi aliyotumwa mwaka jana?

SP said...

vipi CM hizo rufani leo tumeshinda au vipi?