Saturday, October 03, 2009

Chuji huru

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la soka nchini TFF, limempunguzia tena adhabu Athuman Iddi "Chuji" kutoka miezi mitatu hadi mechi tatu, onyo na faini.


Awali Chuji alifungiwa kutocheza soka miezi 3 kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu katika mchezo dhidi ya African Lyon na siku 11 baadaye akafungiwa tena miezi 3 kwa vitendo hivyo hivyo vilivyotokea katika mchezo dhidi ya Majimaji huko Songea.


Yanga ilikata rufaa kwa adhabu ya kwanza ambayo ilipunguzwa na kuwa mechi tatu. Siku chache baadaye Yanga ilikata rufaa kwa adhabu ya pili ambayo nayo imepunguzwa kuwa mechi 3, faini ya 500,000/= pamoja na onyo kali dhidi ya vitendo hivyo.


Kwa hali iliyo, Chuji sasa yupo huru kwani tayari amekosa mechi tatu ambazo ni dhidi ya JKT Ruvu, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar.

5 comments:

John Mwaipopo said...

ila aache ununda. punguzo hilo la adhabu nadhani ni kutokana na sababu za huruma zaidi kuliko zinginezo. wamemwonea huruma tu. aache ununda na aache uswahiba na boban, ndiye anayemfundisha kutumia vitu hatari.

Tina said...

hongera chuji lakini nangalia mpira na sio ubabe.karibu tena kwenye kandada tuendeleze libeneke la soka kwa yanga.

SP said...

vipi mbona kimya leo hakuna update kutoka mwanza?au tumelala tayari.CM weka data basi

Anonymous said...

tukonge roho khakha!!!!!!! nasikia harufu ya myama lazima aliwe muda umefika. Kwako-- CM!!!!!! sijui na nyamagana au wapi?

Anonymous said...

cm lete mambo kaka


ITALY