Tuesday, December 29, 2009

Manji hajajiondoa Yanga - Madega
MWENYEKITI wa Yanga, Imani Madega, amesema ,Yusuf Manji, bado ni mfadhili wa klabu hiyo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Manji aliandika barua kwenda kwa Mwenyekiti wa wazee wa klabu hiyo, Jabir Katundu, kumueleza kuwa ameamua kujiweka pembeni kama mfadhili wa Yanga kwa vile sasa inaweza kujiendesha yenyewe.

Nakala ya barua hiyo ilipelekwa pia kwa Mwenyekiti Madega na Katibu wake Lawrence Mwalusako.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Yanga mtaa wa Twiga na Jangwani jana, Madega alisema hawatambui kujitoa kwa mfadhili huyo kwa vile hajawaandikia viongozi barua ya kufanya hivyo.

Badala yake Madega amewashutumu wazee wa klabu hiyo kwamba ndio wanaoleta chokochoko.

Awali, wazee wa Yanga walimuomba Manji kugombea uenyekiti ambapo aliahidi angetoa jibu Jumamosi iliyopita, lakini badala yake alitangaza kujiondoa kwenye udhamini wa klabu hiyo.

“Manji hajaleta barua kwetu ya kujiondoa yeye amewajibu wazee kama angetaka kujiondoa angetuandikia barua uongozi,” alisema.

“Wazee hao hata hawatambuliki kikatiba ndio waliomfanya Manji ajiondoe Yanga baada ya kumtaka agombee uenyekiti ndipo katika kujibu akajibu na hayo ya kujiondoa,” alisema.

Katika taarifa yake ya mwishoni mwa wiki, Manji alisema kingine kilichomfanya ajiondoe kwenye ufadhili wa Yanga ni namna kocha aliyepita Dusan Kondic alivyoshiriki kufanya usajili mbovu, hali iliyochangia timu yao kufanya vibaya katika mzunguko wa kwanza wa Ligi.

Manji alimtolea mfano mchezaji Honore Kabongo kwamba amesajiliwa kwa fedha nyingi, lakini hakuna mchango wowote aliotoa kwa klabu.

“Nimeamua nijiweke pembeni Yanga, kwa sababu naamini kabisa kwamba ni klabu kubwa na inaweza kujiendesha yenyewe… mimi siwezi kuwa juu ya Yanga,” alisema katika taarifa yake hiyo.

Hata hivyo Manji aliahidi kuendelea kuwa karibu na wachezaji na hata walipotwaa ubingwa wa Kombe la Tusker juzi alikuwa nao.

Tangu Manji kutangaza kujitoa Yanga wanachama mbalimbali, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakiulalamikia uongozi kuwa ndio chanzo cha mambo yote kwa vile ulikuwa mstari wa mbele kutumia fedha nyingi katika usajili ambao haukuleta msaada wowote kwa timu.

Jana mchana wanachama wa Yanga maarufu kama Yanga bomba walikuwa na kikao cha faragha ofisini kwa mfanyabiashara huyo.

SOURCE: HABARI LEO

6 comments:

Anonymous said...

Hii ndio fadhila ya kutegemea mhindi.Tutafute uwezo wa kujitegemea wenyewe.Tuache kuwa tegemezi.Manji ana tu treat anavyotaka kwa sababu tunajidhalilisha sana.Tuna vitega uchumi vya kuweza kujitegemea.Tuchague viongozi wenye upeo wa kupeleka klabu kwenye kujitegemea na sio kina Madega na Mwalusako kazi kukimbilia kuomba Manji aendelee.Akifa leo ndio klabu itakufa???TUTAFAKARI.NAWASILISHA.
MDAU YANGA

Anonymous said...

Lakini Manji si ndo alimleta Kondic na akawa anmlipa yeye isitoshe tulielezwa kwamba usajili wote ulifanywa na Kondic.
Ni kweli kwamba suala la usajili hasa kwa wachezaji wa kigeni wa kigeni liatia kichefuchefu, lakini tatizo si usajili bali ni uwajibikaji wa wale waliosajiliwa, nadhani hakuna mahala wanabanwa endapo mtu hataperform vile ilivyotarajiwa au kwa maelezo mengine mchezaji akishasajliwa basi hakuna namna ya kupima utendaji wake kwa minajili ya kumwajibisha,tuchukue mfano wa karibu wa Mike Barasa tunaona alivyobadilika pale simba sasa tujiulize yanga kulikoni?maana naamini wachezaji wa nje wamepageuza kuwa ni kama shamba la bibi wanakuja pale kuchuma bila kutoka jasho halafu haoooo wanaondoka.
Kama bwana Manji ameamua kujitoa kwa hili nadhani hatendi haki kwa sababu aliyetuingiza mkenge ni Kondic,kusema timu inaweza sasa kujiendesha sio kweli, labda atwambie ameacha vitega uchumi gani endelevu.
Naamini kwa sasa timu kiuchezaji imekaa vizuri kuliko timu yoyote katika ukanda huu maana mpira ulioonyeshwa kwenye michuano ya Tusker sio wa kawaida tofauti na ule wa timu zingine wa kukimbia kimbia na kutegemea individual skills na ushirikina, ni wazi kwamba sasa ndio wakati muafaka wa kupata raha ile tuliyokuwa tunaisubiri kwa muda mrefu endapo hali ya hewa haitavurugika.

Anonymous said...

nyie jamaani manji ana haki sasa mnaanza kumuita eti muhindi ,nyie mmetoa nini kuisaidia yanga ?nothing just bulshit kutukana watu ,mpaka lini manji atatusaidia?hebu kazeni mikanda lipeni ada kama mna uwezo n'go hakuna.

Anonymous said...

anony wa 9:17 acha watu waseme bwana, walio na mapenzi na klabu wanayo haki ya kusema, wenzetu wana 606, kwa bongo hii ndo 606 yetu sasa wasiposemea hapa wakaseme wapi?
mapenzi na klabu siyo lazima utie mkono mfukunoni, watu wanalipa kiingilio ni moja ya support kubwa kwa timu. anayeamua kudhamini timu anajua yuko tayari kusemwa kwa hiyo acha aambiwe.
anapoitwa mhindi ni kutokana na kasumba tu, haimaanishi ubaguzi wala nini.

Anonymous said...

wewe micho kama unasoma hii blog nakuambia wewe ulikua .........wa kimataifa yaani international umeitapeli yanga na wanayanga kwa kumpandikiza dusan kondacta awe kocha wa yanga angalia alivoiharibu yanga amekula ganji kweli kweli.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___