Monday, December 21, 2009

Tusker Challenge Cup 2009

Ratiba ya Nusu Fainali


23 Desemba 2009 : Sofapaka vs Tusker
24 Desemba 2009: Yanga vs Simba

18 comments:

Anonymous said...

Haya hayawi hayawi yawa, mlioona hizi mechi hebu tupeni tathmini ya kila uwezo wa timu. Kwanza inavyocheza na kujipanga, tuweke pempeni ushabiki.CM upo?

Anonymous said...

Mpira tunacheza wa kiwango ya hali ya juu kuliko tulivvyocheza duru la kwanza kwenye ligi...ila hofu yangu ni wachezaji wetu ikija mechi na simba huwa physcological disturbed as wanakuwa na wogo as a result kichwani tayari wankubali leo tutafungwa na simba hence pressure inakuwa high....another issue ni SImba huwa wanakaa pamoja na kujiandaa vizuri hasa hawa jamaa Friends of Simba...anyways tusubiri game...

Anonymous said...

babu wewe ngoja tuu utaona watoto wanavyomkandamiza adui.

Anonymous said...

Naomba uchambuzi wa kiutu uzima au kama wa kisomi, tuache hizi nalinacha ohh wanaogopa jina mmm nataka mtueleze sasa baada ya kukaa na PIPIC je kuna mabadiliko katika uchezaji?

Anonymous said...

tulia kama unanyolewa babu bunduki 3 ziko tayari ngasa,tegete na kigi utanimbia.

Tina said...

umemsahau Ambani bwana,ameanza tena nae mwaka huu!

John Mwaipopo said...

kuna mabadiliko chanya dhahiri. nadhani papic ni bora mara kadhaa kwa kondic

Anonymous said...

Mwanafyale Mwaipopo,
Hebu tupe kinagaubaga ni vipi timu inacheza na wapi umeona mabadiliko makubwa

edwardsikawa said...

Nadhani itakuwa mara ya pili kuandika kwenye hii blog ya wanayanga.Mimi ni Yanga damu na ninapenda kukwambia nimeangalia mechi zote za Yanga,Yanga wamebadilika sana kuanzia beki,viungo na washambuliaji.Yanga sasa hivi wanakaba vizuri yaani beki inajua jinsi a kujipanga hasa baada ya Nadir kurudi,kiungo wanawalisha washambuliaji mipira na kina Tegete,Ngasa na Ambani wako makini sana.Yaani ukiiangalia Yanga ya sasa hivi iko juu sana,Papic ni kocha mzuri japo amekaa na timu kwa muda mchache.

Anonymous said...

Bw Edward,
Maneno matamu sasa tungoje mambo kesho wakati ngozi ikidunda

Anonymous said...

mr edward you are nice to inform us about our club.please keep up todating us ,we are so keen for yanga to kick simbas ass this time.thank you

Anonymous said...

Kesho tukifungwa inabidi turudishe utamaduni wetu wa bakora kwa viongozi utamaduni ambao kwa sasa umeporwa na watani zetu (rejeeni matukio yaliyomkuta Dalali msimu uliopita)alishikishwa adabu na mambo yakabadilika.

edwardsikawa said...

Wala msihofu kuhusu update za klabu yetu ya Yanga.Nitakuwa nawa update kadri ya uwezo wangu.

Anonymous said...

sasa mechi ni saa ngapi?

Anonymous said...

Jamani yaani Manji akiwa mwenyekiti itakuwa vizuri sana. Naona wazee wa Yanga wamejipanga vizuri, sababu Manji akiwa Mwenyekiti, Kifukwe msaidizi, Mwalusako Katibu Mkuu, Kisasa akiwemo ndani uongozi huu utafanya mambo makubwa sana.

Mnyalu said...

It is true kuwa yanga imebadilika kiuchezaji kwani wanamiliki mpira na kugongeana basi zenye akili. Hata hivyo kama wataongeza kasi ya uchezaji kuelekea lango la adui, twaweza vuna magoli mengi mara kwa mara. Kuna improvement ya kutia matumaini haswaa,mnyama ameanza mchecheto na sasa anapanga kutumia mbinu chafu,inshaallah tutapambana naye.

Tina said...

leo ndio leo jamani nawatakia mechi njema wanayanga.

Anonymous said...

tupo pamoja tina na wengineo,inshallah...lazma tumfanye mnyama ubaya baadaye!!