Thursday, January 07, 2010


Ambani, Chuji majaribioni

Wachezaji wawili wa klabu ya Yanga, Boniface Ambani na Athuman Iddi "Chuji" wanatarajiwa kuondoka nchini wiki hii kwenda kwa majaribio kucheza soka la kulipwa.

Ambani anatarajiwa kwenda Afrika ya Kusini kujaribiwa katika klabu ya Orlando Pirates wakati 'Chuji" atakwenda Sweden katika klabu moja ya daraja la kwanza nchini humo.

"Chuji" atakuwa nchini Sweden kwa wiki moja wakati Ambani atajaribiwa kwa wiki mbili.

12 comments:

Anonymous said...

vipi yanga na jamhuri

Anonymous said...

Chuji na Ambani tunawatakiwa majaribio mema na hongera Damas kwa kuwasadia wanandinga wa bongo kupata timu ulaya,big up mwana!

Kigi na Abdullahim Humud wa mtibwa pia wanaonekana kuivaa kisoka,wape jicho ukipata nafasi!

Vipi matokeo ya mechi ya Ivory coast na rwanda?

Anonymous said...

tumechemsha na jamhuri.tumelala 1-0.tunarudi dar kesho.papic amekasirika mno wachezaji hawakucheza vizuri.tumechezesha full team

Anonymous said...

ndio maana wachezaji wa bongo hawapati timu nje kwa sababu hawako serious na kazi yao ,wanacheza chini ya viwango kwa ajili ya fedha ?haya subirini mpaka mwaka 3000.

tina said...

oh sijui tumeshinda tusker vikombe vyote tutashinda.mpira wa bongo hamna kitu.wachezaji wanavuta bangi tu na basi hela tu na pombe.

Anonymous said...

yes you are right hamna uwajibikaji at all

Anonymous said...

Hata Tusker tulibebwa tu.

Anonymous said...

Jamani acheni kuwa vigeugeu kila kukicha.Timu ikishinda huwa mnatoa hongera na pongozi nyingiii...sasa tukifungwa mnakuwa wa kwanza kuponda.
Sio vizuri hivyo kulaumu ila naelewa nyie mashabiki tuu,ila tuliokwisha ucheza mpira tunaelewa matokeo baada ya dk 90.
kwahiyo,tuendelee kuipa timu sapoti na natumaini hatujatolewa kwani katika timu hizo tatu za zenji tumecheza mechi moja tuu mpaka sasa,mnaojua mtuhabarishe vizuri kama tushatoka au la!

Anonymous said...

nyie wote sio wana sipoti mnajua myama kashusha under 20 ktk mashindano haya? ni dharau kubwa sisi kukutana na watoto bora tukawaachia hayo mashindano kimtindo. fungua macho wewe usiwe fala au domo kaya bila ya mahesabu,

Anonymous said...

Wewe ndio domo kaya unayetafuta sababu na visingizio visivyo na msingi.Tuliokuwepo tumeona timu imefungwa kwa kucheza mpira mbovu ndio maana Papic kakasirika sana.

Anonymous said...

jamani hachane hizo

Anonymous said...

Mnyama kashusha Under 20!! Sasa nyie mnacheza mpira ili kuifunga Simba au mnacheza mpira ili kuarchive something?? Ndio maana hatuendelei kila siku tukisha ifunga simba basi aaah kazi imeisha!! Mtakaa hivyo hivyo na umwinyi wenu wa mtaa wa Jangwani. Timu haindelei kila siku mnafungwa Misri,......Fungua macho pipooo!!