Friday, February 12, 2010

Lupopo watua TZ

Wapinzani wa Yanga katika mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika kesho, FC Lupopo, wamewasili jijini Dar es Salaam jana huku wakiahidi kucheza kufa na kupona.

Timu hiyo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, iliwasili majira ya saa 1:00 usiku jana na kupokewa na wadau mbalimbali wa soka nchini.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Erick Katenda, alisema kuwa wamekuja na kikosi cha wachezaji 18 -- wanane wakiwa ni wa kimataifa – mmoja kutoka katika nchi ya Ivory Coast, mwingine Cameroon, wawili Zambia na wanne Zimbabwe.

Katenda ambaye aliwasili nchini tangu Jumatatu, alisema kuwa alishuhudia mechi mbili za ligi kuu ya Tanzania Bara – ya Yanga dhidi ya Mtibwa na Simba dhidi ya Manyema – na kwamba kutokana na kiwango cha wapinzani wao Yanga, hawawezi kuwadharau.

Tutacheza kufa na kupona,” alisema Katenda wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili kwa timu yake.

4 comments:

Revocatus said...

Lazima tuwatooe kwenye reli hao wakongo,naamini wana vijidharau coz wana pesa bt naamini kwa kiwango timu yetu ilipofikia chini ya kostadin papic lazima watatoka vichwa chini pale machinjioni. VIVA YANGA AFRIKA

Anonymous said...

usidharau mwiba ndugu yangu.

lusekelo said...

cha muhimu yanga wasidharau mechi naamini tutashinda kwani jamaa wanafungika tu Mungu ibariki Yanga sc

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___