Wednesday, May 12, 2010

Maftah atakiwa kujieleza
Uongozi wa klabu ya Yanga umemkabidhi barua ya kujieleza beki wake, Amir Maftah na kumtaka awe amejieleza ndani ya siku tatu.

Hatua hiyo imefuatia mchezaji huyo kukaririwa jana na vyombo vya habari akieleza kutoka Mwanza kuwa hawezi kujieleza kwa kuwa hajapata barua ya uongozi wa klabu hiyo.

Alituhumiwa kucheza chini ya kiwango katika mpambano wa kumalizia Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Yanga, Aprili18 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huu mchezaji huyo alionyeshwa kadi nyekundu kwa madai ya kumchezea rafu mchezaji wa Simba kwa makusudi na kuifanya Yanga icheze ikiwa pungufu uwanjani hali iliyotafsiriwa na wengi kuwa amehujumu timu.

Ofisa habari wa klabu hiyo, Louis Sendeu alisema kuwa tayari wamemkabidhi mchezaji huyo barua hiyo ya kumtaka atoe maelezo ya kina ndani ya siku tatu na endapo hatafanya hivyo hatua nyingine za kisheria na kinidhamu zitachukuliwa.

6 comments:

gray said...

ni haki kwa mtumishi/mfanyakazi kutoa maelezo ya kina ikiwa mwajiri / bosi wako kaona utendaji wako wa kazi unatia mashaka. lakini kwa issue ya Maftah Afisa Habari anaikuza kwa radio na magazeti. kwani kupewa barua kwa mfanyakazi ni jambo la kawaida. sendeu mwenyewe alitakiwa apewe barua kwa kuwa kuna wakati anatoa habari si za kweli. mfano siku ya kwanza ya issue ya mhasibu wa yanga na tiketi bandia na wakati wa usajili wa dirisha dogo. anapenda sana kuongea na vyombo vya habari bila kujipanga na kujua kazi zake. mambo ya barua ni mambo ya kiutawala zaidi na mambo ya ndani ya Yanga. mbona hajasema kama Mfadhili mkuu sasa hivi kuna viongozi hawapi cash, mbona hasemi kuhusu madeni ya mwaka jana ya wachezaji kuhusu usajili kilitokea nini?! SENDEU punguza kuongea mambo mengi ambayo mengine ni ya kiutawala. mambo yanayohusu ofisi yako ni mengi sana, mbona huyashughulikii?!

Anonymous said...

Naungana mkono na huyo mdau hapo juu.

Suala la mchezaji kutakiwa kujieleza halikuwa la kutangazwa public kama alivyofanya Sendeu.

Yanga kama waajiri haijamtendea haki Maftah na hapa kuna kila dalili kwamba mwisho wa Maftah katika klabu ya Yanga ndiyo umefika.

Anonymous said...

Usiwahi kusema mwisho wa maftah ndio umefika Yanga.Hakuna sababu ya msingi ya kusema hivyo.Kwanini unasema hivyo? Una sababu zipi za msingi kuja na wazo hilo? Alichokosea afisa habari ni kulikuza swala hilo la kiofisi.

Anonymous said...

Usiwahi kusema mwisho wa maftah ndio umefika Yanga.Hakuna sababu ya msingi ya kusema hivyo.Kwanini unasema hivyo? Una sababu zipi za msingi kuja na wazo hilo? Alichokosea afisa habari ni kulikuza swala hilo la kiofisi.

Anonymous said...

Sendeu anafanya kazi aliyo ajiriwa,kama amekosea mwajiriwake ndiye anajua na siyo sisi tuliopembeni, bora tukae kimya kwa yale tusiyo yajua. Swala la Maftaha mimi linanitia kichefu chefu kama kweli alimpiga Nyoso kichwa kwa makusudi.Mchezaji asiyejua umuhimu wa timu na badala yake anangalia dhamira yake, huyu hana maana. Hawa ndio wana vuta bangi,hebu tukumbuke kwa nini ameachwa timu ya Taifa. Huyu ni zero.

Anonymous said...

Kumpiga kwa makusudi sio kuhalalisha aliyoyasema Sendeu.Sendeu hafai