Friday, May 14, 2010

Ngassa aomba kuhamia Azam FC
Mshambuliaji wa Yanga na timu ya Taifa Mrisho Ngassa amerejea nchini jana na kuiomba klabu yake imruhusu ajiunge na Azam FC ya Dar es Salaam.

Ngassa ambaye alikuwa nchini Rwanda kwa mazungumzo na timu ya APR amesema kwamba dau aliloahidiwa na Azam FC ni kubwa sana na kwa vile soka ndiyo inayompa maisha ya kila siku, si vibaya Yanga wakamfikiria baada ya kuitumikia kwa miaka mitano.

Kuhusu mazungumzo yake na APR, Ngassa amesema dau aliloahidiwa na wanajeshi hao ni dogo kiasi kwamba ni bora abaki nchini ambako kuna vilabu ambavyo vina uwezo wa kumlipa vizuri zaidi.

18 comments:

gray said...

Kwanza natoa Pongezi kwa Ngassa kwa kuchaguliwa mchezaji bora wa Mwaka kwa ligi ya Vodacom msimu uliomalizika hivi karibuni. kwa ukweli naungana mkono na wale waliofanya uteuzi wa mchezaji bora kwani ni haki yake. kila mpenzi wa mpira anajua mchango wa Ngassa kwa Yanga na Taifa Stars. Tatizo ninaloliona kwa wachezaji wetu ni kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu suala la kujitambua au kupotoshwa na wale wanaowaita mameneja wao. ni wazi suala la yeye kuomba kuhamia Azam ni suala la binafsi linalozingatia maslahi binafsi kwa mchezaji kwa minajiri ya kuongeza kipato. sasa anachotakiwa kufanya ni kufuata taratibu zilezile alizotumia wakati wa kusaini mkataba na Yanga. mbona hakuwa anapayukapayuka ovyo kwenye magazeti hadi kwenye magazeti ya Udaku kuhusu usajili wake? ni suala la yeye kukutana na mtendaji mkuu wa Yanga na kumkabidhi barua yake ya maombi ya kutaka kuhama. baada ya hapo asubiri kupewa majibu. maana analalama kwenye vyombo vya habari wakati hata barua yenyewe hajaandika ili aipeleke kwa Uongozi, matokeo yake inaonekana Yanga kama wanambania, wakati sio. kabla hajazaliwa Yanga ilikuwepo na ilishachukua ubingwa mara nyingi sana tu. kwa hiyo kuondoka kwake ni pengo lakini linazibika tu. wachezaji, viongozi punguzeni kuongea sana. mambo mengine ni ya kiofisi zaidi.

Anonymous said...

mwandishi hapo juu umenena na wala hakuna cha kuongezea, nakubaliana na wewe kwa yote. Hivi kwa nini wachezaji wetu hawajifunzi?

Anonymous said...

hayo ndo mambo ya soka la kiprofessional, kama Yanga tunao uwezo wa kuzidi dau aliloahidiwa Azam tumzuie, kama hatuna basi tumruhusu aende, lakini naamini yanga inao uwezo wa kuwapiku Azam nikitilia manani mwaka juzi tulimsajili Kaseja kwa pesa ambazo kwa Tanzania ilikuwa ni rekodi ya juu wakati hakuna mchango wowote wa maana Kaseja aliutoa kwa timu, vipi Ngassa ambaye sisi sote tunajua mchango wake kwa timu.
Siku hizi wanasema HAPENDWI MTU BALI PESA

Anonymous said...

Ameandika barua lakini tunambania.Kama hauwezi kumpa hiyo fedha tumuache ajiunge na Azam kutimiza ndoto zake.Ngassa sio wa kwanza tunaembania.Tufikirie maslahi ya wachezaji.Amehama Ronaldo itakuwa Ngassa???

Anonymous said...

Naamini waandishi wa habari ndio wanaolikuza jambo hili.Kama Azam wameshawasilisha offer yao kwa Yanga ya sh milioni 25, hakuna haja ya kusumbuana.Ni nafasi ya wamiliki wa mchezaji(Yanga) sasa kupima thamani ya mchezaji na kuangalia maslahi ya mchezaji na ya klabu pia kwakua klabu haina biashara zaidi ya kuuza wachezaji.Mimi nafikiri thamani ya Ngassa ni zaidi ya Kaseja wakati ule hivyo ni kuanzia millioni 60 na kuendelea.

Anonymous said...

Ni wakati wa Yanga kuwa makini na mikataba ya wachezaji.Hawa Azam mimi ninawafaham, huwa wanafuatilia mikataba ya wachezaji wote wazuri TFF ikoje ili kama kuna upenyo waweze kuutumia kumpata mchezaji husika.Hivyo ni lazima tujenge utaratibu wa kujadili mikataba ya wachezaji wetu hata katikati ya mikataba kama tunaona mchezaji huyo ni muhimu sana.Barcelona walifanya hivyo kwa Messi, Manchester United nao hivyo hivyo kwa Rooney ili akija mtu anataka kumuuza wapate pesa nyingi sana.Mchezaji ndio utajiri wa TIMU popote duniani

Anonymous said...

Ni wakati wa Yanga kuwa makini na mikataba ya wachezaji.Hawa Azam mimi ninawafaham, huwa wanafuatilia mikataba ya wachezaji wote wazuri TFF ikoje ili kama kuna upenyo waweze kuutumia kumpata mchezaji husika.Hivyo ni lazima tujenge utaratibu wa kujadili mikataba ya wachezaji wetu hata katikati ya mikataba kama tunaona mchezaji huyo ni muhimu sana.Barcelona walifanya hivyo kwa Messi, Manchester United nao hivyo hivyo kwa Rooney ili akija mtu anataka kumuuza wapate pesa nyingi sana.Mchezaji ndio utajiri wa TIMU popote duniani

Anonymous said...

Hapo ndo nitaamini kweli viongozi wetu na huyo sijui ndo mfadhili wetu hamna lolote kwa kushindwa kumzuia Ngasssa kuondoka kwa milioni wakati tulimsajil Kaseja kwa mapesa zaidi ya hayo na hakuna alilofanya, msimu uliopita tulisajili watalii kibao kwa mapesa mengi tu wakaishia kutengeneza vitambi hivi tuko SERIOUS??? au ndio hivyo tena.

Anonymous said...

ujui ,kusajiriwa kaseje zilikua siasa za simba na yanga,ila ilifulia kwenu, kaseja alikua bora simba si yanga, na ataendelea kuwa bora simba na tanzania ,why tunasema viongozi yanga licha na uanasheria wao wa chuo kikuu cha kibaha hakuna walijualo,kama katiba ya yanga ilipitishwa kwa dk 15 bila swali mutaendelea kuwa mbumbumbu milele,mukibisha mumelogwa bye.

Anonymous said...

Ila nyie ni waelevu kw akuchagua mwenyekiti muuza mitumba na sasa mmechagua tapeli ambaye kila mtu tabora anajua, ama kweli nyani haoni kundule

Anonymous said...

nilishasema Azam wakitaka kumchukua Ngassa walete zaidi ya million 60 ndio thamani yake.Na Cannavaro ni million 200.FULL STOP

Anonymous said...

Lengo la blog hii ni kubadilishana mawazo kistaarab. Tunajua hao wanaotumia lugha mbovu ni wale waliozoea kuishi maporini. ni jambo linalosikitisha sana kuona watu mnatumia lugha chafu. kama una maoni au ushauri andika kistaarabu. kama wewe unajijua sio Yanga na lugha ya kistaarabu huna tuachie wenyewe blog yetu.

Anonymous said...

hawakomi hao walipotea sasa wanajileta kidogo kidogo

Unknown said...

Wameanza kuja tena, tuwapokee kwa vidole vitano vitano. tusiwatenge ni wenzetu. tuwaombee angalau kwa mara ya kwanza wapate kunyakua kikombe nje ya ardhi ya TZ. wasicheze mpira wa fitina za kibongo huko wataumbuka kama kwa waarabu, huko hawatabebwa kama walivyozoea. ndo mana hata mara moja hawajawahi kutwaa kikombe chochote nje ya tz.TUNAKUPA TANO MTANI. JITAHIDI

Anonymous said...

Mshambuliaji mahiri wa zamani wa Yanga na pia Taifa stars leo amesaini kuichezea Azam FC kuanzia msimu ujao wa 2010/2011 na atakuwa akilipwa mshahara wa 1.2m kwa mwezi na ada yake ya uhamisho ni 40m. Hili ni pigo kubwa sana kwa Yanga kwa wko mbioni kumpoteza Nadir Haroub Canavaro...

Unknown said...

Paka amla Simba tena

Goli pekee la mshambuliaji wa zamani wa Yanga, John Baraza, juzi liliipa Simba kipigo chake cha kwanza katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati 'Kombe la Kagame', baada ya kulala 1-0 dhidi ya Sofapaka.

Kipigo hicho cha juzi kwenye Uwanja wa Nyamirambo, hapa Rwanda, ni cha pili mfululizo kutoka mabingwa hao wa Kenya, baada ya Simba kugalagazwa 2-1 wakati timu hizo zilipokutana kwa mara ya kwanza katika michuano ya Kombe la Tusker mapema Januari jijini Dar es Salaam na Yanga kuibuka mabingwa wa michuano hiyo.

Kwa ushindi huo, Sofapaka wameungana na wenyeji APR na mabingwa wa Afrika, TP Mazembe, kutinga katika hatua ya robo fainali huku wakiiacha Simba ikihitaji ushindi katika mechi ijayo dhidi ya URA leo ili kusonga mbele, baada ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Atraco, kuzinduka juzi kwa ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya timu ya URA.

Atraco walianza vibaya kampeni za kutetea ubingwa wao baada ya kufungwa kwa bahati mbaya 2-1 na Simba iliyocheza kichovu kama haina kocha katika mechi ya ufunguzi Jumatatu. Sare dhidi ya URA leo, inaweza kuwapeleka mbele Simba, ikiwa Sofapaka watapata ushindi wa asilimia 100 wa hatua ya makundi dhidi ya Atraco.


Shujaa wa Sofapaka juzi Baraza, alipeleka majonzi kwa wana Msimbazi katika dakika ya 31 baada ya mabeki wa Simba kujichanganya na kumpa mwanya mfungaji kupiga shuti lililomshinda kipa Juma Kaseja.


Kipindi cha pili, Sofapaka waliendelea kuliandama lango la Simba na katika dakika 53, Bob Mugalia aligongeana vyema pasi na Hugo Nzoka, lakini Mugalia alipiga shuti ambalo lilidakwa na Kaseja.

Dakika sita baadaye, Sofapaka walikaribia tena kufunga wakati beki Kelvin Yondani alipopiga kichwa 'boko' cha nyuma kwa kipa lakini Nzoka aliyeuwahi mpira huo alishindwa kufunga.

Paka waliokosa magoli mengi, walitaka kuwashangaza Simba kwa goli la ajabu katika dakika ya 87, wakati Kimani alipopiga shuti refu kutokea katikati ya uwanja, lakini Kaseja aliyekuwa amevutika mbele, aliweza kurejea haraka na kuudaka mpira huo.

Anonymous said...

Mie nimechanganyikiwa..lakini poa tu aende Hongera Ngasa asante kwa kuitumikia Yanga

Anonymous said...

Kazi ya mwenyekiti mpya a.k.a tapeli imeanza kuzaa matunda baada ya jana timu hiyo kufungashiwa virago kwa kipigo cha tatu mfululizo huko Rwanda. Waaraabu ni TANO hata hawa wapigana vita nao.
Lakini poa maana mmepata umeme baada ya robo karne gizani.
WALELTE WALETE MKO WAPI, JITOKEZENI KI KWELIKWELI SIYO KUVIZIA. UWANJA UKO WAZI.