Friday, September 03, 2010

Yanga kuhamia Moro?
Sakata la kutumia Uwanja wa Taifa uliyoko jijini Dar es Salaam kwa timu za Simba na Yanga, limechukua sura mpya baada ya Simba kubadili uamuzi wa kwenda Mwanza na kutaka kubaki jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom.

Habari zilizopatikana jana jioni, zinasema kubadili mawazo huko kwa Simba kumepelekea serikali kuinyima Yanga uwanja huo, licha ya kuwepo taarifa za kukubaliwa kuutumia.

Habari hizo, zinabainisha kwamba baada ya vikao vya siku kadhaa kati ya uongozi wa Yanga na serikali kuhusiana na uwanja huo, Yanga ilikubaliwa, lakini kitendo cha watani wao wa jadi kupeleka barua ya maombi kwa siri kimesababisha serikali kubadili uamuzi.

Hatua hiyo, inafuatia Uwanja wa Uhuru kufungwa kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati, hali iliyosababisha timu hizo kongwe nchini kusaka viwanja kwa ajili ya michezo inayozikabili.

Awali serikali ilitoa masharti kadhaa ambayo yaliifanya Simba ibadili mawazo na kuamua kutangaza kutumia Uwanja wa CCM Kirumba ulioko mkoani Mwanza.

Kutokana na hali hiyo, Yanga italazimika kuhamishia michezo yake kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

4 comments:

Gray said...

Inajulikana bayana tabia ya kuwa kigeugeu kwa Uongozi na hata wapenzi wao wa timu yao. ila kwa kiasi fulani Uongozi nao unatakiwa ulaumiwe. huyo Sendeu kila siku unamsikia redioni hata kama taarifa haijakamilka basi kashatangaza ooh tunatarajia hili au lile. ni vema uongozi ukawa na siri na mambo yake. mara kadhaa mambo ya ndani unayasikia nje. kama hili la uwanja, kilichokuwa kinawafanya kila siku msikike redioni ni nini?! mngekaa kimya mpaka kieleweke. kwa kweli mnatuhuudhi sana. sasa mtangaze mapema uwanja ili tuweze kujipanga kwa ajili ya kuifuata timu ya wananchi. Na Sendeu punguza kuongea na vyombo vya habari kama unakuwa HUNA taarifa kamilifu.

Anonymous said...

kweli tanganyika ndio maana maendeleo ya mpira ni duni tataendelea lini ikiwa vilabu mnavyovitumainia ni simba na yanga halafu mnavifanyia ZENGWE la kiwanja mwenye kisu kikali ndie atakae kula nyama wee mkilosa TENGA mpira uliucheza wape mawazo wasomi wenzio ambao hajawahi kugusa mpira ila wanatumia shule kuongoza leo hii unategemea timu hizi mbili kufanya vizuri ktk michezo ya kimataifa? CIAO!!!

Anonymous said...

ctwftxcozguxgtvgrxepx. http://www.acnetreatment2k.com/ - acne treatment
jowksx

Anonymous said...

watanzania tumejitawala?mbona hata kutumia hicho kiwanja mpaka ruhusa itoke ikulu?kwani ikulu iko china?ugabacholi au wahujumu uchumi hawana ukabila wala dini.