Saturday, July 30, 2011

Yanga yaalikwa Sudan

Mabingwa wa soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga itafanya ziara ya siku tano nchini Sudan ya Kaskazini tarehe 5 mwezi ujao ambapo inatarajiwa kucheza na vigogo wa soka wa nchi hiyo El Hilal and El Merreikh.

Huku mchezo wa ngao ya hisani dhidi ya Simba ukikaribia, mechi hizo mbili zitakuwa ni majaribio mazuri kwa Yanga kwa ajili ya kuanza msimu mpya wa ligi. Afisa Habari wa Yanga Louis Sendeu alisema jana kwamba Yanga imealikwa huko Sudan na klabu ya El Hilal.

El Hilal ambayo sasa inashiriki katika Ligi ya Mabingwa Afrika inanolewa na Kocha wa zamani wa Yanga, Milutin Srejdovic 'Micho'.

5 comments:

SHIKABWE MSAFIRI said...

safi sana kwa yanga kupata mwaliko huo.pia kwa ushauri wangu kwakuwa yanga imepata mwaliko huu nakutakiwa kwenda na msafiri usiozidi watu 25,basi mimi kama mdau ningeomba yanga itoe gharama kwa ajili ya wachezaji wengine ili wote katika safari hiyo wawepo wakajifunze kitu kulikoni tu kutegemea watu waliowaalika,wagaramieni wachezaji wengine ili nawao wawepo katika msafara huo,kulikoni kuchagua wachache.

Anonymous said...

babu umenena kweli hiyo ni vizuri na kuwapa morali wachezaji wengine.

Anonymous said...

paulsen ameleta mizengwe,anyway taifa linakuja kwanza.lakini kutokutangaza timu mapema jee hii inakubalika?

Anonymous said...

duh! mvua ya magoli inazidi kunyesha yaani polisi dodoma katufungulia gati mpaka leo magoli yanazidi ,duh mshikaji unaona vipi?
je uongozi bomu?
jee unaona wachezaji bomu?
au kocha bomu?
hebu tuanze kuchambua kabla hatujakutwa na mauti.

Anonymous said...

jamani tupeni raha leo tuliopo nje hatuna mawasiliano mengine ila hii blog mkereketwa wa yanga kuwait