Friday, March 30, 2007

Kambi ya Yanga:
Siri Kubwa..............


Kambi ya Yanga kwa ajili ya kujiandaa na pambano la raundi ya pili kuwania ubingwa wa Afrika dhidi ya Esperance bado imekuwa siri kubwa.

Inasemekana kwamba kikosi cha timu hiyo kinatarajia kuondoka nchini kwenda katika nchi mojawapo ya Kiarabu kwa ajili ya kuweka kambi. Yanga huenda ikaweka kambi katika moja kati ya nchi za Libya, Misri na Qatar ili kuzoea mazingira yanayofanana na ya Tunisia ikiwemo kucheza mechi za usiku.

Yanga imeweka mbinu ya kutotangaza mahali itakapoweka kambi kwa kuhofia timu ya Esperance kutuma wapelelezi wake pale itakapokuwa imeweka kambi. Inasemekana wiki chache zilizopita, timu ya soka ya Tanzania - Taifa Stars iliathirika dhidi Senegal baada ya kuitangaza sana kambi yake huko Brazil.

Safari njema wana-Yanga.No comments: