Monday, April 02, 2007

Amir Maftah ruksa CAF, Mahadhi aumia

Waziri Mahadhi

Shirikisho la soka CAF limemruhusu Amir Maftah kuichezea Yanga katika michuano ya Klabu bingwa Afrika mwaka huu.

Yanga ilichelewa kukamilisha uhamisho wa ndani wa Amir Maftah, hali iliyosababisha CAF nayo kuchelwa kuleta kibali chake cha kuichezea Yanga katika michuano hiyo.

Kuruhusiwa kwa Maftah kutaimarisha kikosi hicho kwani mchezaji huyo ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani.

Amir Maftah yupo katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania - Taifa Stars.

Naye kiungo mahiri wa Yanga, Waziri Maftah ameumia na hatajiunga na kikosi cha Yanga katika safari ya Tunisia.

Hata hivyo huenda akacheza katika mechi ya marudiano baada ya wiki mbili.

2 comments:

Anonymous said...

Waziri Mahadhi (Mandieta)! Tumuombee apone haraka. Kuhusu mechi na Esperance YANGA tuna kila sababu ya kushinda. Tuzidi kuomba Mungu ili tucheze ligi ya mabingwa.

saklde said...

Hongera sana ndugu yangu Amir,na pole sana kwa kuumia naamini uko fit sasa,naomba tufunguliwe unaikumbuka hii hahahaha!