Tuesday, April 03, 2007

Yanga yapaa...
Mwaikimba, Mukenya wabakiGaudence Mwaikimba

Kikosi cha Yanga kimeondoka nchini jana mchana kuelekea Tunisia bila ya wachezaji wake wawili tegemeo Gaudence Mwaikimba na Edwin Mukenya.

Wachezaji hao wawili wameachwa kwenye safari hiyo na Kocha Milutin Sredjovic "Micho" kutokana na kuchelewa kujiunga na kambi ya timu hiyo. Kuchelewa huko kumechukuliwa kama kitendo cha utovu wa nidhamu, hivyo wachezaji hao watalazimika kubaki nchini kusubiri kikosi hicho kirejee kutoka Tunisia.

Mukenya alikuwa anatoka kwao Kenya ambako aliitwa kuichezea timu yake ya Taifa - Harambee Stars dhidi ya Swaziland wiki iliyopita wakati Mwaikimba alirejea nchini na Taifa Stars kutoka Senegal lakini baada ya kutua nchini akasafiri kwenda kwao Mbeya kushughulikia masuala ya kifamilia.

Micho amewalaumu wachezaji hao kwamba wamewaangusha wana-Yanga kwa kitendo hicho cha kuchelewa kuripoti lakini hata hivyo anakwenda na kikosi chenye wachezaji wazuri wanaojituma na wenye nidhamu.

Yanga pia itamkosa Waziri Mahadhi "Mendieta" ambaye amebaki kutokana na kuwa majeruhi. Pia Kocha Micho hatakuwepo katika benchi la ufundi la timu hiyo.

Kikosi hicho kimeondoka na kiongozi mmoja Yusuf Mzimba. Viongozi wengine wataondoka leo kwenda Tunisia wakiongozwa na Imani Madega.

Mungu Ibariki Yanga.

No comments: