Thursday, April 05, 2007


Mungu Ibariki Yanga


Mabingwa wa soka Tanzania - Yanga inatarajiwa kuingia uwanjani Ijumaa usiku kupepetana na Esperance ya Tunisia katika pambano la Klabu Bingwa ya Afrika.

Pambano hilo litakalofanyika katika Uwanja wa Olympique d'El Menzah linatarajiwa kuwa gumu hasa ukizingatia kwamba Yanga imepania kukata uteja kwa timu za Kiarabu na Esperance itataka kuwatuliza mashabiki wake baada ya hivi karibuni kuchapwa na wapinzani wao wa jadi Etoile du Sahel 3-1.

Kocha Micho anatarajiwa kutangaza kikosi ambacho kitakuwa na malengo ya kujihami zaidi hasa ukizingatia kwamba Esperance wana washambuliaji wenye uchu mkubwa wa ufungaji mabao. Habari zisizo rasmi zinasema kwamba tayari Micho ametanga za kikosi ambacho niIvo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Hamis Yusuf, Nadir Haroub, Amir Maftah, Credo Mwaipopo, Amri Kiemba, Hussein Swedi, Mrisho Ngassa, Said Maulid na Abdi Kassim.


Kila la heri Yanga. Mungu Ibariki Yanga na Tanzania kwa ujumla.
2 comments:

Anonymous said...

kikosi kinatia matumaini. tuombe ushindi ili tucheze ligi ya mabingwa.

Anonymous said...

Mimi nina swali hivi Gula Joshua Super Sub ana matatizo gani mbona siku hizi hachezi.?? Kuna mtu yeyote ana sababu za kiufundi?