Saturday, April 07, 2007

ESPERANCE 3 YANGA 0
Esperance jana ilitubamiza mabao 3-0 katika mchezo ambao mwamuzi kutoka Misri alichangia kwa kiasi kikubwa kuidhoofisha Yanga.
Yanga ilicheza na wachezaji pungufu kwa muda mwingi wa mchezo huo baada ya beki wake tegemeo Hamisi Yusuf kupewa kadi nyekundu katika dk15 tu ya mchezo. Ilikuwa ni kadi yake ya pili ya njano.
Katika kipindi hicho cha kwanza mchezaji wa Yanga Said Maulid SMG aliumizwa na ilibidi aingie Thomas Mourice. Hadi mapumziko mabao yalikuwa 1-0.
Mabao ya Esperance yalifungwa na Kamel Zaiem(dk 28), Amine Ltifi (65) na Walid Tayeb (72).
Katika mchezo huo wachezaji Nadir Haroub, Amri Kiemba, Amiri Maftah, James Chilapondwa, Abuu Mtiro na Abdi Kassim walionyeshwa kadi za njano kwa makosa mbalimbali ikiwemo la wachezaji wa Esperance kusingizia kuuumizwa vibaya.
Kikosi cha Yanga kilipangwa kama ifuatavyo; Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Wisdom Ndlovu, Nadir Haroub, Hamisi Yusuf, Amri Kiemba, James Chilapondwa, Abdi Kasim, Amiri Maftah, Gulla Joshua/Abuu Mtiro na Said Maulid/Thomas Mourice.
Hakuna kukata tamaa, tujikusanye na sisi tuwapige 4-0 tuingie kwenye Ligi ya mabingwa. Mapambano yanaendelea.
Yanga inatarajia kutua nchini Jumatatu ijayo.

1 comment:

Anonymous said...

Bado kuna matumaini ya kuwafunga hawa watunisia. Waliweza kutushinda kwao kimizengwe ila mchezo wao niliuona hauridhishi hata kidogo. jamani tuishabikieni timu yetu mwanza