Thursday, April 12, 2007

Ivo matatani kimajungu majungu

Kipa namba moja wa Yanga na Taifa Stars - Ivo Mapunda anatuhumiwa kutoa ombi kwa viongozi wa Klabu hiyo "kununua" waamuzi kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Klabu Bingwa Afika kati ya Yanga na Esperance utakaofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Akihojiwa na kituo kimoja cha redio Jijini Dar es Salaam, Ivo alidai kwamba soka ni ndani na nje ya uwanja, hivyo ni vizuri viongozi wa klabu yake kuangalia uwezekano wa kucheza soka la nje ya uwanja kama viongozi wenzao wa vilabu vingine vya nje ambavyo wamekwishakutana navyo (Petro du Luanda na Esperance) walivyofanya.

Hata hivyo Ivo ambaye alikuwa anayachukulia maoni hayo kiutani utani, anashangaa kuona anashikiwa bango na wadau mbalimbali wa soka hususan wale wa timu moja yenye upinzani wa jadi na Yanga. Inavyoonekana wengi wana uchungu kuona Ivo anaendelea kuwa TZ 1 kiasi cha kuanza kuhoji ni vipi Ivo amefungwa magoli mengi ndani ya mechi chache. Sasa na sisi wadau wa Yanga tunahoji, je kipa wa klabu kubwa kama AS Roma ya Italia ambaye alifungwa 7-1 naye hafai? Mpira unadunda jamani, leo unaweza kuwa na clean sheet, kesho ukafungwa.

Endeleza makamuzi Ivo Mapunda, wewe bado ni TZ 1. Makipa wengine inawezekana bado wapo honeymoon ya mwezi mzima hadi wanasimamishwa na Klabu zao.

1 comment:

Anonymous said...

madai yote hayo yanakuzwa na Simba kwa vile wanaona kipa wao Kaseja amewekwa benchi na Ivo. Kaseja mwenyewe hivi sasa kafungiwa, sasa sijui hao simba wanaleta majungu ya nini?