Saturday, April 14, 2007

Aibu, aibu, aibu
* Mchezaji asimamishwa kwa kupewa red card

Inasemekana kwamba uongozi wa klabu ya Yanga umemsimamisha mlinzi tegemeo wa klabu hiyo, Yusuf Hamisi kwa madai ya kuhujumu timu katika mechi dhidi ya Esperance.

Yusuf alionyeshwa kadi nyekundu katika mechi hiyo katika dk ya 15, hali inayowapa mashaka viongozi wa klabu hiyo na hata kocha Micho. Katika mechi hiyo, wachezaji wengine sita wa Yanga walilambwa kadi za njano lakini hakuna tuhuma zozote dhidi yao achilia mbali kipa Ivo Mapunda ambaye alifungwa magoli mawili ya kizembe katika mechi hiyo.


Beki huyo mahiri ambaye kutokana na umahiri wake katika ulinzi pia anajulikana kama Waziri wa Ulinzi, ameshangazwa na hatua hiyo ya kusimamishwa na mbaya zaidi anasema kuna watu wanamshangaa kwamba hajaomba radhi kwa kupewa kadi nyekundu.

Kwa hali inavyoonyesha ni kwamba kwa sasa bado soka la Tz lina safari ndefu sana. Kama mchezaji akipewa kadi nyekundu katika mechi ndiyo anafungiwa, basi hata wachezaji wengine watakuwa wanaogopa kukaba maadui ili bora wafungwe goli kuliko kumkaba mchezaji kwa kuhofia kadi ambayo inaweza kumsababisha afungiwe na klabu yake.


Kwa mtaji huu viongozi wa Yanga mmechemka. Sasa Hamisi Yusuf afungishe Yanga kwa faida ya nani? Yeye mwenyewe alikuwa anapambana ili kuitetea Yanga ifanikiwe kusonga mbele na kuingia katika hatua ya makundi ambayo mchezaji anaweza kuonekana na mawakala wa vilabu vikubwa vya nje na kujipatia timu Ulaya au kwingineko.
Tuwape moyo wachezaji wetu. Hata huko kwenye ligi za Ulaya kadi nyekundu zipo lakini wachezaji hawasimamishwi na vilabu vyao.

Mungu Ibariki Yanga.

1 comment:

Anonymous said...

Mimi sitaki kumlaumu Hamis Yusufu kwa ile kadi ya pili na nyekundu juu yake, lakini pia tusilaumu tuu kocha na viongozi kwa uamuzi wao.

Ni ukweli kuwa timu ilidhoofika kutoka na zile kadi, sasa naamini viongozi wanajaribu kuwafunza wachezaji kuwa makini ktk mashindano makubwa kama hayo. Naamini hujuma inayoongelewa (hasa na kocha) sio ya kwamba Hamis alichukua hela ili afungishe timu, bali kuwa hakuwa makini baada ya kupewa kadi ya kwanza, jambo ambalo liliiumiza timu.

Namuomba Hamis na wenzake wauchulie uamuzi juu yake positively. Hata huko ulaya, chukulia mchezaji acheze rafu 3 in 15 minutes of the game, na apewe red card. Hiyo itachukuliwa kuwa sabbotage (not bribery) ambayo kwa kiswahili ndo wanaita hujuma...

Kila la kheri Yanga in the coming match.