Saturday, April 14, 2007

Ligi ndogo ya TFF kuanza leo


Yanga leo inajitupa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kupambana na Moro United katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi ndogo ya TFF.

Ligi ya mwaka huu ambayo itakuwa katika makundi matatu ya Arusha, Morogoro na Dodoma imekosa mdhamini, hali ambayo huenda ikasababisha ligi hiyo kukosa msisimko na timu kucheza kwa ajili ya kulinda heshima zaidi.

Ligi hiyo itakayodumu kwa miezi miwili, imeandaliwa katika kipindi hiki cha mpito ambacho TFF inataka kwenda sawa na mfumo wa ligi wa nchi nyingi duniani. Ligi nyingine rasmi inatajiwa kuanza mwezi Julai na kumalizika Mei mwakani.

Yanga ipo katika kundi ambalo litacheza mechi zake katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid huko Arusha pamoja na timu za Moro United, AFC na Polisi ya Morogoro.

Kila la heri Yanga.

No comments: