Thursday, April 19, 2007

Esperance hao ndani ya TZ


Esperance wakijiaandaa kuondoka Tunis
Photo Courtesy of EST website

KIKOSI cha timu ya soka ya Esperance tayari kimetua Dar na leo kinatarajiwa kuelekea Mwanza kwa ajili ya pambano la marudiano la raundi ya 3 ya Klabu Bingwa ya Afrika utakaochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini humo.

Esperance imekuja na wachezaji 21 huku ikiwa imewaacha wachezaji wake tegemeo 4 kwa sababu mbalimbali ikiwemo adhabu pamoja na majeruhi. Wachezaji hao ni Kamel Zaiem, Zied Bhairi, Michael Eneramo na Souheil Berradhia. Waamuzi wa mchezo huo kutoka Zimbabwe - Kenias Marange atakayesidiwa na Alfred Zindove na Cosmas Nyoni nao tayari wamewasili kwa ajili ya pambano hilo.

Haya sasa, jamaa ndiyo wameshakuja. Tuendelee na mazoezi na Inshalah Mungu akitujalia siku hiyo game likikaa fresh tumalize kazi. Au siyo wadau wenzangu?

3 comments:

yafricans said...

Sorry lakini vijana wetu walishalala. Kilichobaki sasa ni kujiandaa kucheza Confed Cup. Matokeo ya kesho
Yanga 2
Esp 1 (win 4-2agg)
Mungu ibariki Yanga!!!

Anonymous said...

Hakuna lisilowezekana katika soka. Game linaweza kuwakataa Esperance, tukabaki tunastaajabu ya Musa.

Anonymous said...

Kweli kabisa anonymous Said... sorry, anonymous hapo juu. Tunahitaji kuwa fighting spirit, na kutokata tamaa hadi dakika ya mwisho. Sasa kama na vijana wakikata tamaa kama sisi wapenzi unadhani hata huko confed. cup tutabaki?

Lazima tupigane kufa na kupona na inshahla, esperance wanaweza ondoka...