Wednesday, April 18, 2007

Mkono wa salamu kwa Esperance

Katika hali inayoonyesha kwamba ni salamu kwa Esperance, Yanga imeibamiza AFC kwa mabao 5-0 katika mchezo wa ligi ndogo ya TFF iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid huko Arusha.

Yanga ilipata mabao yake kupitia kwa Abuu Mtiro, Credo Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba (2) na Abdi Kassim.

Yanga inatarajiwa kuondoka leo kwenda Mwanza ambapo Jumamosi ijayo kupambana na Esperance katika Uwanja wa CCM Kirumba kwenye mchezo wa marudiano wa raundi ya 3 ya Klabu Bingwa Afrika. Katika mchezo huo Yanga inahitaji ushindi wa 4-0.

3 comments:

CM said...
This comment has been removed by the author.
Anonymous said...

vipi, huyo mtu wa msimbazi alisemaje..?

Ila sasa ni wakati wa kuacha ushabiki wa kishamba. Wote tushangilie magoli ya Yanga, moja hadi lingine.

Mimi natabiri magoli matatu kwa Yanga hadi half time. Moja toka mwa Mwaikimba, Tomas Moris na lingine la Abdi Kasim.

Kipindi cha pili najua kina Ngasa na wengineo watamalizia kazi.

Kila la Kheri chama langu. Mungu Ibariki Yanga, Mungu ibariki Tanzania, AMEN.

yafricans said...

Sorry Bro hizo ni ndoto. Yanga si kama Man U alivyofanyizia Roma.

God bless Yanga & Liverpool!