Tuesday, April 17, 2007

Leo ni AFC na Yanga

Ligi ndogo ya TFF itaendelea leo na kwenye kituo cha Arusha, Mabingwa watetezi Yanga itaingia uwanjani kupambana na AFC ya Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Yanga huenda ikatumia mchezo wa leo kujaribisha makucha yake kabla ya kupambana na Eserance mwishoni mwa wiki hii. Hata hivyo Yanga imewasimamisha wachezaji wake kadhaa kutokana na utovu wa nidhamu, wachezaji hao ni Hamisi Yusuf, Emmanuel Switta, Lulanga Mapunda. Wachezaji Edwin Mukenya na Gaudence Mwaikimba wamefunguliwa lakini huenda wasipangwe kutokana na kile kinachodaiwa "kutokuwa katika hali nzuri kimchezo".

Wakati huo huo, Yanga imemsimamisha meneja wa timu hiyo Robert Ekerege. Nafasi ya Ekerege inatarajiwa kujazwa hivi karibuni.

No comments: