Saturday, April 28, 2007

Yanga kuivaa Moro Utd leo

Yanga inaanza mzunguko wa pili wa ligi ndogo ya TFF kwa kuumana na Moro Utd katika mchezo wa Kundi A wa ligi hiyo utakaofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid huko Arusha.

Yanga inaingia katika mchezo wa leo ikiwa imepatwa na balaa la majeruhi. Wachezaji Nadir Haroub, Waziri Mahadhi, Edwin Mukenya, Gula Joshua, Said Maulidi na Hamisi Yusuf wote huenda wakaukosa mchezo wa leo kutokana na kuwa majeruhi na wengine kuwa wagonjwa.

Katika mchezzo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya 0-0.

Yote juu ya yote ni kwa kikosi kilichosalia kufanya kweli ili kujipatia pointi 3 muhimu leo.

Kila la heri Yanga.

No comments: