Monday, April 30, 2007

Tumeshindilia 4-0

Yanga imeishindilia Moro United 4-0 katika mchezo wa ligi ndogo ya TFF.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Gaudence Mwaikimba, Mrisho Ngasa, Amri Kiemba na James Chilapondwa.

Katika mchezo huo, Ivo Mapunda alirejea golini baada ya kukaa benchi kwa mechi tatu mfululizo.

Yanga sasa inahitaji pointi moja tu ili iingie hatua ya sita bora ya ligi hiyo.

No comments: