Wednesday, May 02, 2007

Yanga 1 AFC 0

Yanga imefanikiwa kuingia katika hatua ya sita bora ya ligi ndogo ya TFF baada ya kuitungua AFC 1-0 katika mchezo uliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid huko Arusha.

Bao pekee la mchezo huo ambao Yanga ilikosa mabao mengi ya wazi, lilifungwa na Thomas Mourice katika kipindi cha pili.

Yanga itaondoka leo kwenda Mwanza kujiandaa na mchezo wake dhidi ya El Merreikh siku ya Jumapili ijayo.

No comments: