Thursday, May 03, 2007

El Merreikh watua Dar
El Merreikh ya Sudan imewasili nchini jana na kikosi cha watu 33, wachezaji 21 na viongozi 12 tayari kukwaana na Yanga katika mchezo wa kwanza wa raundi ya 4 ya michuano ya Kombe la Shirikisho la barani Afrika.

Kocha wa timu hiyo Otto Pfister anaamini kwamba mpira utakuwa mgumu na mwamuzi ni ndani ya dakika 90.

Timu hiyo inajivunia wachezaji wao wa kulipwa kutoka Nigeria, Mali na Togo ambao ni Endurance Idahor, Efosa Eguakun, Jean-Paul Abalo na Boubacar Kone.

Hapana shaka vijana wetu hawatatishika na majina ya nchi wanazotoka hawa wachezaji wao wa kulipwa.


2 comments:

Anonymous said...

Kocha wao anaongelea mechi ya marudiano, huenda wamekuja katika mkao wa kutafuta sare halafu watuchijie kwao.

La muhimu kwa Yanga ni kupiga mabao mengi hapa nyumbani, la sivyo tutakuwa tumejikaanga wenyewe.

Anonymous said...

Kweli lakini inabidi tukubali kwamba Yanga safu ya ushambuliaji sio nzuri. Tukiweza kupata ushindi wa bao mbili bila kufungwa na kujihami huko Sudan tunaweza kusonga mbele. Wenzetu wanawachezaji kutoka Brazil, Nigeria na Togo na kocha mzuri. Matokeo ya jumapili
Yanga 2 Wasudani 1
Mungu ibariki Yanga.