Friday, May 04, 2007

Majeruhi kibao Yanga

Yanga inakabiliwa na majeruhi kibao siku chache kabla ya kupambana na El Merreikh ya Sudan katika mchezo wa kwanza wa raundi ya 4 ya Kombe la Shirirkisho barani Afrika CAF.

Kwa mujibu wa Kocha mkuu wa timu hiyo Milutin Sredojevic "Micho", Yanga itawakosa wachezaji kadhaa ambao ni majeruhi na wengine wamefungiwa.

Katika orodha ya wachezaji majeruhi wamo Waziri Mahadhi, Gula Joshua, Hamisi Yusuf na Saidi Maulidi. Majeruhi wengine ambao wapo 50/50 kucheza ni Credo Mwaipopo na James Chilapondwa. Aidha Shadrack Nsajigwa na Abdi Kassim watakuwa nje ya dimba kutokana na kuwa na kadi mbili za njano. Pia wachezaji Lulanga Mapunda na Emmanuel Switta wanatumikia adhabu ya utovu wa nidhamu waliyopewa na klabu hiyo.

Yote juu ya yote bado tuna kikosi imara ambacho kinaweza kupangwa kama ifuatavyo:

1. Ivo Mapunda
2. Fred Mbuna
3. Abdul Mtiro
4. Wisdom Ndhlovu
5. Nadir Haroub "Cannavaro"
6. Edwin Mukenya
7. Amir Maftah
8. Amri Kiemba
9. Gaudence Mwaikimba
10.Thomas Mourice
11. Mrisho Ngassa

Subs: Ben Haule, Hussein Swedi, Abuu Ramadhani

Wadau mnaonaje kikosi? mmekuwa kimya saaaaaana. Mpo kweli wandugu?

Mungu Ibariki Yanga na Tanzania yetu.


4 comments:

Anonymous said...

Kikosi kimekaa vizuri. Kama kikiandaliwa vizuri ki-saikolojia kinaweza kufanya vizuri. Tukiombee tuu kikosi hao watakaopangwa wawe fiti siku hiyo.

Ila wadau mnaonaje hawa wakazi wa Mwanza wanaoikatisha tamaa timu kwa kuzomea, kutoingia uwanjani n.k? Kwani hawajui kuwa kupelekewa mechi ya kimataifa ni favour tu? Kwanza hawana hata timu ligi kuu.

Ni wakati sasa wapenzi tujitokeze kwa wingi na kuishangilia timu toka mwanzo hadi mwisho, ili vijana wapate nguvu. Tusisubiri tuu mabao. Kelele za mashabiki nazo ni muhimu psychologically. Hivi haiwezekani kuanzisha vikundi nya ushangiliaji kama ilivyokuwa muchacho cha watani zetu?

Mungi Ibari YAfrica, tupate walau matokeo ya 3 - 0 ...

Positive Living...

Anonymous said...

Mkubwa!
Wadau wa hili chama tupo na bloguni tunapita daily.
Sasa nina mawazo mawili:-
Kwanza nitafurahi kama utakuwa unatuwekea matokeo ya mechi za yanga ontime after mchezo.
Pili, hawa wasudani wanafungika hawa. Kocha wao ni wa kawaida tu. Vijana watulie ili angalau tupate hizo $.

CM said...

nashukuru kwa mapendekezo yako anony2.
Nitajitahidi kutuma matokeo ya mechi za Yanga mapema kwa kadri nitakavyojaaliwa kuwa karibu na computer.

Amani ikae nanyi, mzidi kutmbelea blog hii na kuwasilisha maoni yenu.

Anonymous said...

Wanachama tupo sana mzee usikate tamaa, taratibu tutafika. hapa naandika najua mechi limeanza lakini ndio hivyo tena matokeo natarajia toka hapa hapa, tupe mapema mzee.