Sunday, May 06, 2007

Sare ya 0-0 tena

Kwa mechi ya nne mfululizo Yanga imeshindwa ku-score goli baada ya kutoka sare ya 0-0 na El-Merreikh ya Sudan katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Ikicheza mbele ya mashabiki walioingia uwanjani hapo bure baada ya mchezo huo kununuliwa kwa sh. milioni 100 na mfadhili wa timu hiyo Yusuf Manji, Yanga ilikosa mabao mengi kiasi cha kuwakatisha tamaa mashabiki wake waliokuwa wamefurika uwanjani hapo.

Mchezaji Yosso Mrisho Ngassa ndiye aliyekuwa akifurukuta lakini krosi alizokuwa akizipiga zilikuwa mara nyingi zinaokolewa ama washambuliaji wa Yanga walikuwa wanapiga mashuti hafifu golini.

Yanga itabidi ijilaumu yenyewe kwa kukosa mabao mengi ya wazi, hali inayoiweka timu ya El Merreikh kuwa kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele kwani timu hiyo haijawahi kupoteza au kutoka sare katika michezo yake ya nyumbani.

Katika mchezo wa leo Yanga iliwakilishwa na:

1. Ivo Mapunda
2. Fred Mbuna
3. Abdul Mtiro
4. Wisdom Ndhlovu
5. Edwin Mukenya
6. Credo Mwaipopo
7.James Chilapondwa/Hussein Swedi
8. Amri Kiemba/ Abuu Ramadhani
9.Thomas Mourice
10.Amir Maftah/Said Maulidi
11.Mrisho Ngassa

Lakini katika soka lolote laweza kutokea. Ila Yanga kazi ipo.

4 comments:

Anonymous said...

Kweli ndugu yangu, ktk soka lolote linawezekana. Lanini nadhani tumejiweka ktk wakati mgumu saana kuweza kuwatoa wale jamaa.

Ingawa hawatishi saana, lakini wakiwa nyumbani kwao naamini mechi itakuwa ngumu sana kwetu. Labda tu tujipange na tujiandae vema tena mwakani. Ingawa Yanga tutakuwa na advantage kuwa sare yoyote ya magoli inatuvusha, lakini wale jamaa wanaonekana wana nguvu saana (physique) kuliko wakwetu.

Labda tukiwa na kina Nsajigwa na Abdi Kasim, tutaweza kuwachaganya.

Mungu Ibariki yanga na Tanzania. hakuna kukata tamaa.

Anonymous said...

nafikiri Mwaikimba angekuwepo ndiyo angefukuzwa kabisa Yanga. Bora ambavyo hakuchezeshwa.

Anonymous said...

Inabidi tukubali kwamba timu yetu siyo nzuri hasa katika safu ya ushambuliaji. Mwaikimba amepata lawama zote lakini wenzake hawana hafadhali. Kilichobaki ni kujitahidi kujihami huko sudan na kusajili 'mastriker' kwa ajali ya robo fainali. Yanga bado yaweza kusonga mbele.
Yanga 2 El Mereikh 2.

Anonymous said...

Kimpira badoooooooooo ! Sijui tufanyweje ili tuepukane na mikosi kama hii. Hakuna wa kumtupia LAWAMA bali hatujui mpira wa kisasa