Monday, May 21, 2007

Tumetolewa, nini kifanyike?

Kwanza nawapa pole sana kwa kutoweza kutuma post weekend hii hali iliyosababisha mgongano wa mawazo hususan katika matokeo ya mchezo wa Yanga na El Merreikh. Kwa usahihi ni kwamba tumefungwa 2-0.

Sasa tupo nje ya hii michuano, ni muda wa kujipanga upya. Je, nini kifanyike kwa ajili ya msimu ujao kama tukipata nafasi ya kuwakilisha nchi katika michuano ya Afrika?


Kazi kwenu wadau wa Yanga.

5 comments:

Anonymous said...

tununue washambuliaji mahiri kutoka nje. Hawa tulionao wameshindwa kufunga goli hata moja katika mechi 5.

Jaduong Metty said...

Kwani hii ni mara ya ngapi kwa Yanga kufanya vibaya? Kama Yanga hawakutatua matatizo yao 1990, hawawezi kutatua ya leo.

Tatizo kubwa ni uongozi. Hii si kwa Yanga au Simba tu, ni uongozi nchi nzima. Kama Tanzania ilivyo na rasilimali kibao, Yanga nayo ina rasilimali moja kubwa - jina lake - lakini kutokana na mawazo finyu ya viongozi pamoja na wanachama na washabiki, wanaYanga wanaishia kuzitazama tu Arsenal, Chelsea, Manu, etc zikipeta kwenye luninga.

Nimekuwa nifuatilia kwa makini "kelele" za kocha Micho. Kikubwa anachokipigia kelele ni ukosefu wa nidhamu wa "mastaa", ambao mara nyingi wanakingiwa vifua na viongozi. Tofauti kubwa kati ya Micho na viongozi uchwara wa michezo Bongo ni kwamba anaelewa umuhimu wa "attitude" kwenye mafanikio ya mtu,shirika, au hata timu ya mpira.

Siyo kwamba Yanga hawana washambuliaji. Kwani baadhi yao wanacheza timu ya Taifa? Tatizo ni "attitude" ambayo haiwezi kubadilika kama mawazo ya Mtanzania wa kawaida - wakiwemo viongozi wetu na wachezaji, bado ni ya kitoto na mafupi.

Anonymous said...

Nakubaliana kabisa na Jaduong Metty. Bila kubadilisha attitude za wachezaji na viongozi wetu, tutabadilisha makocha hadi aje Mzee Fergie wa ManU, lakini matunda hatutayaona.

Wachezaji wetu wako short sighted. Wanajiona super-stars wakati hamna lolote. Jana nimesoma eti wachezaji wanasema watafanya sherehe endapo Micho ataondoka. Hawajui kuwa kuwa na kocha kama Micho ni kwa faida yao wenyewe pia.

Kwa attitude zao hizi ndio maana Tanzania haina mchezaji yeyote ulaya. Nonda Shaaban alipitia Yanga miaka hiyo, wakati yeye bado anacheza kwenye Premiership hadi leo, timu nzima ya wachezaji aliokuwa nao Yanga (kina Lunyamila etc) hakuna hata mmoja ambaye bado yuko uwanjani... tayari wameisha. Kisa... uzembe wa mazoezi, ulevi, ngono, kutozingatia maadili ya uchezaji, etc).

Ndio maana kwenye uchaguzi unaokuja inabidi tuchague viongozi wenye fikra mpya. Sio tu viongozi wa miaka ya 70 na 80, eti kwa vile waliwahi kuifunga Simba. Simba sasa hivi sio focus yetu. Focus iwe mbali saana, kwenye klab bingwa Afrika.

Then, wakati wa usajili Micho apewe nafasi asajili wachezaji anaotaka, bila kuingiliwa na kiongozi yeyote, halafu tumpime uwezo wake baada ya hapo, basi. Sasa hivi tutakuwa tunamwonea kusema timu haija-perform wakati wachezaji wote aliwakuta na tabia zao tunazielewa...

JM.

Anonymous said...

Wachezaji wa Simba walisherehekea kuondoka kwa mbrazil Nielsen Elias, na wakasema Patric Phiri ni bora mara 10 ya Elias (according to magazeti). Kwa mtu mwenye akili timamu, huwezi kulinganisha kocha ambaye ameshakaa kwenye benchi la ufundi na timu ya taifa ya Brasil kwenye World Cup na kocha ambaye hata hajawahi kuipeleka timu yake kwenye semi-finals za Africa Cup.

Kinachoonekana hapa ni kuwa wachezaji wetu wanataka kocha mshikaji, ambaye haulizi mtu asipokuja mazoezi na anakubaliana na visingizio vya kila namna, mara nimeuguliwa na mjomba, mke ,shangazi, n.k. Huyo kocha atapendwa na kusifiwa na wachezaji wetu (Tanzania) wengi.

Solution nadhani pia ni elimu. Yanga iweke lengo kuwa ktk kipindi cha miaka 5 ijayo, wachezaji wote wawe na walau elimu ya kidato cha 6 na kuendelea. Hawa bila shaka watakuwa na aspirations za kufika mbali, kucheza Ulaya n.k. badala ya kulewa visifa uchwara na kuanzisha majungu kwa walimu walio serious kazi zao.

Ni hayo tuu kwa sasa.

Anonymous said...

JM,
Ulichosema sina cha kuongezea, maana nikikumbuka akiwa Yanga Nonda hakuwa mshambuliaji wa kutisha kama akina Lunyamila, lakini wako wapi sasa? wanapandisha mabega kabla hawajacheza mpira. Micho ni kocha kweli, analosema hawafundishiki hilo halina utata, goli walizokosa nina uhakika angekuwepo Mwalala angefunga, lakini huyu Crouch wetu ni uchafu mtupu