Friday, May 18, 2007

Uchaguzi wa Yanga kuahirishwa?

Suala la nani ana haki ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa klabu ya Yanga linatarajiwa kuamuliwa na wanachama wa klabu hiyo Jumapili ijayo.

Utata wa haki ya kupiga kura umejitokeza baada ya muafaka uliofikiwa na klabu hiyo mwaka jana kuwa na mapungufu makubwa ambayo hayaelezei kipengele hicho cha uchaguzi hali inayowapa wale wenye kadi za mwaka 1992 pekee kuwa na haki ya kupiga kura.

Kwa kutambua hilo, Ofisi ya michezo ya wilaya Ilala imesimamisha zoezi la kutoa fomu na kuwataka wana Yanga kukutana Jumapili kuamua mustakabali wa wapiga kura. Tayari ofisi hiyo imesema ipo tayari kuendelea na utoaji wa fomu endapo wanachama hao wataafikiana kuhusu suala hilo siku ya Jumapili.

Napenda kupongeza hatua hii ya Ofisi ya michezo Ilala kwa kutambua kwamba wakiendelea kung'ang'ania kutoa fomu, watasababisha mgogoro mkubwa. Kama suala hili lingeendelea, wanachama wengi wangekuwa wametengwa kushiriki kwenye uchaguzi jambo ambalo lingeleta makundi ndani ya klabu.

Ni juu ya wanachama wa Yanga kutumia busara siku ya Jumapili. Hatma ya klabu ipo mikononi mwa hao watakaoshiriki katika mkutano wa Jumapili.

Yanga Imara, Daima mbele.


2 comments:

Anonymous said...

Hata hao wanachama ambao wanatambulika na katiba ya mwaka 1992 hawana uhalali wa moja kwa moja kwa sababu hawajalipia ada ya uanachama kwa miaka mingi.

Inabidi hapo wanachama wakae na kutatua haya mapungufu.

Anonymous said...

Kweli kabisa.

Kwa vile kuna muafaka, wanachama wake wakubaliwane kufanya uchaguzi kwa kazi zote zilizopo.

Pili: Hivi inawezekana kupata wasifu binafsi(CV) za hao wanaoomba kuchaguliwa na maelezo ya nini wanataka kuifanyia Yanga kwenye hii blog? Hilo ni la muhimu saana, maana mtu asiye na vision ataonekana dhahiri.

Mimi nadhani Yanga (hata Simba) hazipaswi kutegemea wafadhili ambao siku wakiondoka zinarudia umaskini wa kutupa. Zinapaswa kujiendesha zenyewe, mfadhili naye awe na shares , hata kama yeye ndo atakuwa na 90% shares poa.

Yanga inao wapenzi zaidi ya Million 3 ktk tanzania naamini. Sasa hawa wakihamasishwa kuwekeza walau sh. 1000 kila mwaka (alfu moja tu kila mmoja) yanga itakuwa na uwezo wa kukusanya sh. billion 3 kila mwana. Hii ina maana Yanga inaweza kukopa fedha benki na kujenga Wanja kama la Mkapa pale Jangwani baada ya miaka michache tuu.

Sasa Viongozo watarajiwa wakipewa nafasi ya kuweza agenda zao hadhani tutapata watu saafi wasiotakata kujinufaisha na vihela vya mapato ya milangoni au hela za Mfadhili.

Kila la kheri yanga.