Thursday, May 24, 2007

Usaili wakamilika, majina kutoka leo


Usaili kwa ajili ya wagombea uongozi katika kalbu ya Yanga ulikamilika jana na ofisi ya Michezo ya Wilaya ya Ilala inatarajiwa kutoa majina ya waliofanikiwa kupita katika usaili huo.

Wakati Yanga ikielekea kwenye uchaguzi, mchuano mkali unatarajiwa kuwepo kwenye nafasi za juu za Mwenyekiti na Katibu Mkuu.

Kwenye nafasi ya Mwenyekiti, wagombea wanaopigiwa chapuo la kuchukua nafasi hiyo ni Imani Madega na Mbaraka Igangula. Madega kitaaluma ni mwanasheria na ni Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Pwani na pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF. Aidha Igangula kitaaluma ni msanifu wa majengo na amewahi kushika nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti wa klabu hiyo miaka ya nyuma.

Katika nafasi ya Katibu Mkuu nako patakuwa hapatoshi kwani miongoni mwa wagombea wa nafasi hiyo, kuna majina kama Lucas Kisasa na Costantine Maligo.

Hebu tutegee sikio Ofisi ya Michezo ya Wilaya itoe majina tuone songombingo litakavyokuwa Jumamosi.


Sisemi sana nisije nikaambiwa napiga kampeni.

Wakati huo huo, mfadhili wa klabu hiyo, Bw Yusuf Manji ametoa posho ya 20,000/= kwa kila mwanachama kwa ajili ya nauli ya kuja kushiriki uchaguzi mkuu wa hapo kesho katika ukumbi wa Karimjee.
1 comment:

Anonymous said...

Asante kwa updates na kila la kheri kwa wale watakao-shiriki uchaguzi. Mwisho wa siku kuna kushinda na kushindwa. Watakaoshindwa washirikiane na washindi kuijenga Yanga. Sii wote tutakuwa viongozi kwa wakati mmoja. Lakini michango yetu wote (ya hali na mali) ni muhimu saana hata tukiwa nje ya uongozi. Watakaoshinda nao wahimize umoja na mshikamano wa wapenzi na wanachama wote klabuni.

Ila sasa na wale walochukua mshiko wa nauli za uchaguzi kesho kweli waende kuchagua viongozi. Wasije wakatia 20,000 kibindoni na kesho wasitokee Karimjee. Ningekuwa Mimi ndo mfadhili, ningewaambia kila wanachama wakutane kwenye tawi lao, na wakodi basi hadi ukumbini kisha nawalipa wenye mabasi... ahaaa....