Wednesday, June 20, 2007

Athumani Iddi huru.......kutua Yanga


Mgogoro wa muda mrefu wa kimkataba kati ya mchezaji wa kiungo Athumani Iddi na klabu ya Simba ulifikia tamati juzi baada ya Shirikisho la soka nchini TFF kutotambua mkataba huo.

TFF ilitoa muda wa mwezi mmoja kwa klabu ya Simba na Athumani Iddi kumaliza tofauti zilizopo kwenye mkataba ambapo Athumani Iddi alimtuma mwakilishi wake (msuluhishi) kutoka Tanganyika Law Society(TLS) akutane na klabu hiyo, lakini viongozi wa Simba hawakutaka mjadala kuhusu suala hilo kwa vile wanachama wa klabu hiyo tayari walikuwa wameamua kufunga mjadala wa mchezaji huyo katika mkutano mkuu wa dharura wa klabu hiyo iliyokutana miezi miwili iliyopita.

Athumani Iddi aliamua kujiengua Simba kutokana na Simba kushindwa kutekeleza yale yaliyo ndani ya mkataba na pia kuingiliwa 'mambo binafsi'.

TFF iliingilia kati baada ya kuona mchezaji huyo kupitia TLS hapewi ushirikiano na viongozi wa klabu hiyo. Pia TFF kama chombo cha kusimamia mpira nchini ililazimika kumuokoa mchezaji huyo ambaye alikuwa tegemeo katika timu ya Taifa ya Tanzania - Taifa Stars asipotee wakati bado mchango wake kwa Taifa unahitajika sana.

Iddi tayari ameweka bayana kwamba klabu ambayo atachezea baada ya kutoka Simba ni Yanga.

Tunakukaribisha kwa mikono miwili Athumani Iddi "Chuji" lakini ujue kazi ipo kwa Micho.No comments: