Monday, June 18, 2007

Tunaanza na Mtibwa


Shirikisho la soka nchini TFF limetoa ratiba ya ligi ndogo hatua ya sita bora ambapo Yanga itaanza kampeni hiyo kwa kufungua dimba na Mtibwa Sugar katika kituo cha Arusha.

Mtibwa ambayo ni moja ya timu iliyotoa wachezaji wengi katika timu ya Taifa ya Tanzania - Taifa Stars, inanolewa na Mkenya James Aggrey Siang'a ambaye atakuwa na kumbukumbu nzuri ya kocha wa sasa wa Yanga Micho ambaye mwaka 2003 akiwa SC Villa ya Uganda na Siang'a akiwa Simba walitwangana makonde uwanjani wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame ambapo Simba ililala 1-0.

Ratiba ya mechi za Yanga katika hatua hiyo ni:

Juni 23: Mtibwa Sugar
Juni 27: JKT Ruvu

Marudiano
Juni 30: Mtibwa Sugar
Julai 4: JKT Ruvu

Mshindi katika kundi hili atacheza na mshindi wa kundi la B lenye timu za Simba, Ashanti na Polisi Morogoro ambazo zitacheza katika kituo cha Morogoro katika mchezo wa kutafuta bingwa wa nchi katika michuano ya Afrika.

Mshindi wa mchezo huo atawakilisha nchi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika wakati atakayeshindwa kwenye mchezo huo atawakilisha kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho - Afrika.

No comments: