Friday, June 15, 2007

Jack Lloyd ChamangwanaKuna mdau mmoja aliuliza kuhusu Jack Chamangwana:

Ni kwamba kocha huyo alikaririwa mwezi uliopita na magazeti hapa Tz akisema kwamba tayari ana majina ya wachezaji yosso aliowakusanya kutoka katika ligi ya Coca Cola hatua za mwanzo kutoka mikoa mbalimbali na sasa anachosubiri ni fainali za michuano hiyo ya vijana (Coca Cola) ili aunde kikosi kamili.


Bila shaka tunaelekea lakini ninachohofia ni ile tabia ya binadamu kutothamini cha kwako mpaka jirani yako akuonyeshe. Inasemekana mchezaji kama Henry Joseph alifanya mazoezi pale Jangwani akiwa yosso lakini hakuonekana mpaka alipokuja kuibuliwa na Simba na sasa ni kiungo tegemeo wa timu ya Taifa.

Umakini unahitajika katika kuibua vipaji na huenda ukimya wa Jack Chamangwana ukawa ni wa kutafakari kikosi chake cha vijana mahiri wenye vipaji ambao watakuwa tishio siku za usoni.

Kila la heri Jack Lloyd Chamangwana katika shughuli zako.

No comments: