Tuesday, June 12, 2007

Tunabaki A-Town

Yanga imepangwa katika kundi A ya Ligi ndogo ya TFF hatua ya sita bora itakayocheza mechi zake katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid huko Arusha.

Yanga ambayo awali ilikuwa katika Jiji hilo katika michezo yake ya mwanzo ya ligi ndogo, imepangwa kundi moja na timu za Mtibwa Sugar pamoja na JKT Ruvu.

Katika kundi B litakalocheza mechi zake Morogoro, timu za Simba, Ashanti na Polisi Morogoro watakuwa wakitafuta nafasi moja ya kuwakilisha nchi katika mechi za Kimataifa mwakani.

Timu mbili zitakazoshika nafasi za juu katika kila kundi zitachuana ili kupata Bingwa wa nchi ambaye atakuwa mwakilishi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati atayeshindwa katika mechi hiyo ataingia katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Kazi ipo hapo.


No comments: