Wednesday, September 26, 2007

Ligi 'kuanza' leo?
Yanga ya Dar es Salaam huenda 'ikaanza' ligi leo katika Uwanja wa Mkwakwani huko Tanga pale itakapopambana na wenyeji wao Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom iliyoanza mwishoni mwa juma lililopita.
Ushindi kwa Yanga leo ni muhimu katika kujenga kujiamini katika ligi hiyo baada ya kuangukia pua katika mcezo wake wa ufunguzi dhidi ya Ashanti United kwa 1-0.
Coastal Union ambayo hujulikana kama Wagosi wa kaya, walianza ligi hiyo vizuri kwa kuifumua Simba kwa 1-0 hivyo leo itataka kudhihirisha kwamba haikubahatisha kuwaangusha vigogo hao. Coastal Union hivi sasa ipo chini ya mchezaji wa zamani aliyewahi kuchezea vilabu hivyo viwili (Yanga na Coastal) - Joseph Lazaro.
Mechi nyingine zitakazopigwa leo ni ni pamoja na Simba na Polisi Moro katika Uwanja wa Jamhuri Mororgoro, Prisons itakayoivaa Ashanti kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Kagera itakayoikaribisha JKT Ruvu mjini Bukoba.
Kama kawaida yetu tutakuwa tunajulishana hapa chini katika comments kile kinachoendelea ndani ya dk.90. Kadri mchezo unavyoendelea mnaweza kupitapita kucheki comments kama kutakuwa na mbadilliko ya matokeo.
KIla la heri wana Jangwani.

7 comments:

Anonymous said...

Mpira ni mapumziko bado ni 0-0.

Anonymous said...

Duh, yasije tokea tena yale ya Moro. ..

Anonymous said...

Tumepigwa tena moja. Mpira umekwisha

Anonymous said...

Timu nadhani apewe Jack. Wakati wake timu ilikuwa haifungwi ovyo ovyo hivi. Kila mtu duniani ana kundu na bahati yake. Kwa ili Jack ana bahati. Na akipewa mapesa kama hawa wengine na usaidizi kidogo tutaenda mbali.

Mfano yeye alikuwa anampenda sana kudra Omari. Kumbe kweli ni mchezaji mzuri.

Nimepoteza uvumilivu. 2 loss mfululizo is an acceptable

Anonymous said...

Kwa kweli. There should be a problem somewhere. Siamini kuwa timu iliyosajiliwa kwa ajili ya kupambana na kina Esperance mwakani inafungwa kienyeji na Ashanti na Coastal Union, bila kujitetea.

Tatizo litafutiwe ufumbuzi mapema.

Anonymous said...

Kilichotuponza ni ufundi.
1. Wachezaji hawakuandaliwa kuwa fit kuanza kucheza. Walitakiwa wafanye mazoezi ya kupata pumzi kwanza na sio kwenda kuruka ruka pale bandari

2. Wachezaji wako wengi na wote wana aina tofauti za uchezaji. Benchi la ufundi limeshindwa kutafuta combination nzuri ya kuwafanya wacheze kitimu

3.Tactics pia tuko ovyo. Mfano mechi ya Ashanti tulitumia nguvu ili tupate magoli lakini bahati tukawa hatuna. Baadae tukachoka kwa sababu hatuko fiti tukafungwa.

4. Tanga hali kadhalika. Nguvu sana wakati hatufiki nazo mwisho.

5. Saikolojia pia iko ovyo. Viongozi wamewajenga wachezaji kujiona wao ni wazuri zaidi. Hivyo wakibanwa tu kidogo wanafrustrate

6. Kocha kutokuja mapema pia ni tatizo.

Tukirekebisha hayo tutafanya vizuri.

MAKA PATRICK MWASOMOLA said...

Simba na Yanga ni timu zinazoongozwa na waswahili na wahuni amini maneno yangu hapo katika hizo timu hata kama akija Tele Santana kocha wa zamani wa Brazil mfumo uliopo katika hizo timu ni kuwa kama marefa na TFF hawatazibeba zitaendelea kuchukua vichapo tu.Nazipoenda sana hizi timu lakini wana mfumo dume na hawataki kusoma alama za nyakati ili wabadilike.Mpira siyo maneno mpira kazi na vitendo.Asante.